Kwa mara ya kwanza duniani roboti imetumika kumfanyia upasuaji wa macho mgojwa. Upasuaji huo ulifanyika kwa mafanikio na huwenda katika siku za usoni roboti wakatumika kwa wingi kumfanyia mtu upasuaji.
Madaktari wametumia roboti ya kwanza kufanya upasuaji wa macho na kurejesha uwezo wa kuona kwa mgonjwa kwa mara ya kwanza duniani. Teknolojia ya sasa inayotumia mionzi ya kichungua (laser scanners) inasaidia madaktari kuweza kugundua magonja yanayosumbua retina.
Kundi la madaktari kutoka hospitali moja nchini Uingereza, walitumia roboti hiyo kutoa ngozi nyembamba zaidi kutoka kwenye jicho la mgonjwa.

Kwa kawaida madaktari hutumia njia ya kupunguza mapigo ya moyo yanayokwenda kwenye retina ili kuweza kutibu retina lakini ilionekana kuwa kwa matumizi ya roboti ilifanya kazi hiyo kwa urahisi zaidi.
Madaktari hao walitumia ‘joystick‘ na touchscreen nje ya jicho la mgonjwa kuiongoza roboti hiyo wakati upasuaji huo ukifanyika.

Upasuaji huo ulikuwa ni muhimu kufanyika kwa sababu ngozi hiyo ilikuwa ikiendelea kukua jambo ambalo lingeweza kumsabishia upofu. Mpaka ngozi hiyo inatolea ilikuwa na udogo wa milisentimita takribani 100.
Mgonjwa huyo mwenye umri wa miaka 70 aliyefanyiwa upasuaji huo sasa anasema anahisi vyema. Madaktari wana matumaini kuwa mfumo huo utasaidia katika upasuaji unaohitaji umakini zaidi.
Vyanzo: The guardian, BBC