fbpx
Afrika, Afya

Njia mpya ya kujikinga na maambukizi ya VVU kwa wasichana kufanyiwa majaribio Afrika

kujikinga-na-maambukizi-ya-vvu-kwa-wasichana-majaribio
Sambaza

Watafiti nchini Marekani wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika majaribio ya njia mpya na ya kwanza kwa wanawake kuweza kujikinga dhidi ya maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi na sasa utafiti huo kuamia barani Afrika.

 maambukizi ya VVU kwa wasichana kufanyiwa majaribio Afrika

Kifaa hicho ambacho kina umbo la duara, plastiki na kinachovutika kitaweza kukaa ndani ya sehemu za siri za mwanamke na kuweza kuachia taratibu mchanganyiko wa madawa yenye uwezo wa kuua vijidudu vya VVU wakati wa kujamiiana.

INAYOHUSIANA  Safaricom yapigwa faini ya mamilioni kwa sababu ya huduma mbovu
Uwekaji

Kifaa hicho chenye umbo la mduara/pete kinaurefu wa inchi mbili na kitakaa katika eneo la ‘cervic’ ndani ya uke.

Mwaka 2012 tayari wanasayansi walipata matokeo ya uwezo mkubwa wa teknolojia hii kuzuia maambukizi katika nyani na baada ya hapo utafiti zaidi kwa wasichana wa kike nchini Marekani uliendelea – NPR.

Ingawa kifaa hicho kitaitaji kubadilishwa kila baada ya miezi sita wengi wanaona kitasaidia sana kwa mabinti kwani ni mara nyingi huwa wanajikuta katika wakati mgumu kuwalazimisha wanaume kuvaa mipira/kondom.

INAYOHUSIANA  Sidiria kwa ajili ya kugundua saratani ya matiti. #Afya

Kwa vijana waliotumia kifaa hichi huko nchini Marekani walisema hakiathiri kabisa ‘utamu’ wa tendo la ndoa. Na kuna ambao walisema wenza wao waliona kama ndio kimeboresha zaidi tendo hilo – kwani tayari kwa muda mrefu wengi wanaamini kondom zimekuwa zinaathiri tendo hilo.

Kifaa kimepewa nafasi ya zaidi ya asilimia 75% kuweza kuzuia maambukizi ya VVU.

Je wewe una mtazamo gani na teknolojia hii? Tuambie kwenye ene la comment na usisahau kusambaza makala ya TeknoKona kwa marafiki.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |