Inapata mwaka sasa tangu Infinix ilipoachia Infinix Zero Ultra, leo tutangalia simu mpya aina ya Infinix Zero 30 5G ambayo ndio simu ya kwanza kwa kampuni ya Infinix kuja na mabadiliko makubwa katika kipengele cha camera ikiwa na 4K 60fps.
Utangulizi:
Infinix Zero 30 5G ilizinduliwa Septemba katika nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania. Toleo hili la kipekee linalenga jopo la watu wa hali zote wenye utamani mkubwa wa kujiendeleza kupitia utengenezaji wa kontenti za filamu/video kitaalamu tunaita ‘Vlogger’. Kupitia makala hii utafanya maamuzi juu ya simu hii ambayo inapatikana kwa bei ya Tsh. 1,060,000 tu kwa sasa.
Kamera:
Ingawa kijadi mimi huanza kwa kuzungumza juu ya kamera za nyuma za simu nyingi, katika kesi ya Zero 30, nitafanya ubaguzi. Hii ni kwa sababu ina uwezo wa kurekodi video za 4K 60fps na ’50MP AF Vlog kwa Camera ya mbele wakati si simu nyingi zenye hadhi ya juu (flagship) huzingataia kipengele ambacho kiukweli kinawatumiaji wengi. Nilifanya jaribio la uchukuaji video na picha katika nyakati tofauti kupitia camera ya mbele na nimeridhishwa utendaji kazi wake.
Simu hii nyuma ipo na Kamera tatu, Kamera kuu ni Megapixel 108 apertures f/1.7 na PDAF + OIS pamoja kamera saidizi ya Megapixle 13 yenye Ultra wider sensor na Megapixel 2 yenye tertiary sensor.
Utendaji na Software:
Zero 30 5G inatumia chipset ya MediaTek Dimensity 8020 yenye CPU ya octa-core (cores nne za 2.6 GHz Cortex-A78 super na cores nne za 2.0 GHz Cortex-A55) na Arm Mali-G77 MC9 GPU. Dimensity 8020 SoC hushughulikia kazi nyingi kwa urahisi na hadi za ujazo wa GB21 RAM (12GB iliyojengwa ndani + GB9 RAM yaniongeza), kutenda kazi kwa wepesi bila kuhofia programu ngapi zinafanya kazi wakati mmoja vile vile ina mfumo wa kupoza simu isipate joto, unaojumuisha tabaka 11 za nyenzo za kupoza.
Muundo na Display:
Zero 30 5G ina unene wa mm 7.9 tu ni rahisi kukaa mfukoni lakini pia fremu zake za pembezoni ni mahiri si rahisi kuvunjika.
Muundo wa juu wa display ni FHD+ ya inchi 6.7 (pikseli 2,400×1080) onyesho la 3D lililopinda la AMOLED na kiwango cha kuonyesha upya/Refresh rate hadi 144Hz lakini pia inapanel na unaweza fanya machaguo 60Hz, 120Hz au 144Hz ambayo ni smooth zaidi.
AMOLED hufanya kazi nzuri katika kushughulikia weusi na kama unavyoweza kutarajia, paneli mahiri hufanya kazi nzuri katika kuonyesha maudhui ya media titika. Onyesho hutoa mwangaza wa kilele wa niti 950, ambayo huhakikisha utazamaji mzuri hata nje chini ya jua moja kwa moja.
Maisha ya betri na kasi ya kuchaji:
Ikiwa na uwezo wa betri wa 5,000mAh na usaidizi wa kuchaji kwa haraka/fast charge wa W68, Zero 30 5G iko katika aina ya simu ambazo zinapaswa kuchajiwa hadi mwisho wa siku baada ya kuchaji asubuhi, haswa ikiwa unatumia skrini kwa refresh rate 144Hz na matumizi ya kimtandao. Ikiwa unatumia simu kwa kiwango cha chini cha kuonyesha upya/refresh rate, kuna uwezekano utakaa zaidi ya siku. Walakini, kwa kuwa kasi ya kuchaji inayotolewa hapa ni ya haraka sana, mchakato mzima hauonekani kuwa mgumu kama unavyofanyika kwa simu zingine.
Ufupisho:
- Muundo maridadi wenye paneli ya ngozi laini (leather) upande wa nyuma unahisi vizuri mkononi
- Onyesho maridadi la 144Hz lililopindika hutoa uzoefu mzuri wa kutazama
- Simu hutoa utendaji thabiti na wa kuaminika
- Kurekodi video ya 4K 60fps inayotolewa na kamera ya mbele (selfie) ni kipengele hadimu
- Gharama nafuu kulinganisha na simu za makampuni mengine zenye features sawa na hii.
Tembelea mitandao ya kijamii ya @infinixmobiletz au wapigie kwa nambari 0656317737
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment je toleo hili umelipokeaje? na je linaweza likaleta ushindani mkubwa katika soko?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.