fbpx
Apple, apps, Teknolojia, whatsapp

WhatsApp kutopatikana tena kwa Mamilioni ya simu! Fahamu kama simu yako itakubalika

whatsapp-kutopatikana-kwa-mamilioni-ya-simu

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

WhatsApp kutopatikana tena kwa mamilioni ya simu za Android na iOS ifikapo mwaka 2017. Uamuzi wa WhatsApp umetokana na simu hizo kuwekwa kwenye kundi la simu za zamani sana na hivyo kutohimili mambo mapya yanayowekwa kwenye app hiyo.

WhatsApp wanaomilikiwa na Facebook, wamesema wataanza taratibu kuacha kutuma masasisho (updates) kwa mamilioni ya simu duniani kote ifikapo Januari mwaka huu.

whatsapp WhatsApp kutopatikana

Kundi la kwanza litakaloathirika ni simu za Windows, Android na iOS, na pia kufikia mwezi wa sita mwaka 2017 simu zitakazoathirika na uamuzi huo zitaongezeka, wataongeza zingine za BlackBerry, Nokia S40 na Nokia Symbian S60.

INAYOHUSIANA  App 5 Za Kuingia Nazo Mwaka 2016

Kupitia blog yao wamesema sababu kuu ni kwamba simu hizi za zamani hazina uwezo wa kuendana na teknolojia za kisasa zinazoletwa ndani ya matoleo ya kisasa ya WhatsApp.

App ya WhatsApp ilianza kupatikana rasmi mwaka 2009, na hadi sasa inawatumiaji zaidi ya bilioni 1. Mwaka 2009 wakata wanaanza zaidi ya asilimia 70 ya simu ambazo app hii ilikuwa inafanya kazi ilikuwa ni za Nokia na BlackBerry.

INAYOHUSIANA  Takwimu za Tanzania na uhalifu wa kwenye mtandao #Uchambuzi #Ripoti

Ni simu gani zitaathirika?

Whatsapp kutopatikana

Kwa simu za Android inajumuisha simu zote zinazotumia toleo la Android 2.1 na Android 2.2. Kwa simu za Windows ni simu zote zinazotumia toleo la Windows 7. Kwa iPhone ni simu zinazotumia iOS 6, kama iPhone yako inaruhusu kusasisha (upgrade) basi fanya hivyo kwenda toleo jipya – ila kwa iPhone 3GS ambayo iOS 6 ndio mwisho basi kwao WhatsApp ndio ‘bye bye’.

INAYOHUSIANA  R.I.P Internet Explorer : Kivinjari Kipya cha Windows Kinakuja

Wenye muda hadi Juni 2017: BlackBerry OS, BlackBerry 10, Nokia S40 na Nokia Symbian S60.

‘Uamuzi huu ni mgumu sana kwa sisi kuuchukua ila ni uamuzi sahihi ili kuweza kuwapatia watu njia bora zaidi ya kuwasiliana na marafiki, familia na wapendwa wao kwa kutumia WhatsApp’ – maneno yaliyosemwa na WhatsApp

Vipi umeuchukuliaje uamuzi huu? Je simu yako ipo salama?

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |