fbpx

Honor 9N yazinduuliwa

0

Sambaza

Mwaka 2018 Honor ambayo ipo chini ya Huawei wameonekana wakitambulisha simu kadha wa kadha baada ya miezi michache tu kupita na siku chache zilizopita wametoa simu rununu nyingine.

Simu za Honor kwa asilimia kubwa zinafanya vizuri katika soko la ushindani na hii pengine inasababishwa na uwekezaji ambao unakuwa umefanyika katika simu husika hivyo kuwa katika nafasi nzuri kuweza kuuzika kwa haraka.

Honor 9N imeshatambulishwa na kwa haraka haraka kuna utofauti mdogo lakini wa muhimu ukijaribu kulinganisha na simu janja iliyotoka kabla yake (Honor 9i). Je, Honor 9N ina sifa gani?

Muonekano/Kioo. Simu hii ina umbo la herufi “V” kwenye uso wa mbele lakini ambao unaufanya kioo kionekanake chote. Kioo chake kina urefu wa inchi 5.84 ya kiwango ubora kabisa.

INAYOHUSIANA  Huawei yaizidi Apple kimauzo

Kipuri kinachoendesha simu (processor). Hapa Honor 9N imewekwa HiSilicon Kirin 659 SoC lakini kwenye uzinduzi huo ilibainishwa kuwa wana mpango wa kuboresha kipuri (kwa simu zao zijazo) na kutumia GPU Turbo kwa ajili ya watu kufurahia wakati wanapokuwa wanacheza gemu.

Honor 9N

Inatumia kadi mbili za simu.

Kamera. Katika kipengele hiki wameweka kamera mbili upande wa nyuma ambazo zina MP 13MP+2MP pamoja na LED flash na kwa mbele wameweka kamera yenye MP 16 ikiwa na uwezo wa kutambua sura (kutumia sura kama njia ya usalama).

RAM/Memori ya ndani. Tofauti na simu iliyopita na ya sasa ipo hapa na zipo aina tatu tofauti; RAM GB  3+GB 32-Diski uhifadhi, RAM GB 4+GB 64-Memori ya ndani na RAM GB 4+GB 128-Diski uhifadhi.

INAYOHUSIANA  Xiaomi yaendelea kukua kwa kasi

Betri/Programu endeshi. Oreo ndio toleo la programu endeshi lililowekwa kwenye Honor 9N na kwa upande wa betri ina 3000mAh.

Honor 9N

Aina toufati za rangi kwenye simu rununu ya Honor 9N.

Kuanza kuuzwa ni mpaka Julai 31 na bei yake kwa 3GB RAM+32GB ROM ni $174|Tsh. 400,200, 4GB RAM+64GB ROM ni $1203|Tsh. 466,900 na 4GB RAM+128GB ROM ni $261|Tsh. 600,300.

Vyanzo: GSMArena, India Times na Gadgets 360

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.