Dunia imekuwa ni kijiji na pale unapohitaji kufahamu kitu mtandaoni basi sio kitu cha ajabu kutafuta majibu mtandaoni na basi ni lazima utatumia kitu kinachoitwa “Kivinjari” (Mozilla, Opera Mini, Safari, n.k) ambacho kinasimama kama moja ya nyenzo ya kufanikisha kupata kile ambacho unaktafuta kwenye mtandao.
Imekuwa sehemu ya maisha yangu kwamba karibu kila inapoitwa leo basi lazima niperuzi huku na kule kutafuta vitu kwenye ulimwengu wa kidijiti na nimekuwa nikiwa karibu kutaka kujua vitu vingi ambavyo vinaweza kurahisisha matumizi yangu ya muda kwenye intaneti.
Kama utakuwa ni mpekuzi kama mimi utakuwa umegundua kuwa kwenye kivinjari cha Mozilla Firefox kuna kipengele kipya kinachoitwa “Firefox Send” ambapo utaweza kuweka na kusambaza/kuwashikisha na wengine kile ambacho utakuwa umekiweka huko lakini mchanganuo wake uko hivi:
- unaweza ukapakia kitu cha mpaka ukubwa wa GB 1 bila ya kuwa akaunti kwenye kivinjari hicho (Firefox) au ukaweza kuweka kitu cha mpaka GB 2.5 kisha ukasambaza kiiungo (link) ili waweze kuona/kupakua kile ulichokiweka huko,
- uwezo wa kuamua ni mara ngapi wanaweza kushusha kile ambacho umewashikisha lakini haizidi mara 100 kwa kila mtu. Pia unaweza ukaweka muda ambao ukipita kiungo husika kinakuwa hakiwezi kufanya kazi-kiungo kinaweza kudumu mpaka muda wa juma moja (siku 7),
- unaweza ukaweka ulinzi kwa kuweka nenosiri kwa kile ambacho umekipakia huko; utakayekuwa umempa nywila ndio atakuwa na uwezo wa kuona/kupakua ulichomsambazia.
Firefox Send inatofautiana na Dropbox kutokana na kwamba ukipakia kitu kule basi kitakuwa huko mpaka pale utakapoamua kwenda kukiondoa. Kupata huduma hiyo ya BURE BOFYA HAPA. Vipi unazungumziaje kitu hicho kipya kwenye kivinjari cha Mozilla Firefox?
Vyanzo: GSMArena, Mozilla