Unaifahamu App ya Tiketi Mtandao? Kama hauifahamu ondoa shaka maana Teknokona leo tumekuandalia maelezo yote ya muhimu kuhusu App hii. Tiketi Mtandao ni App ya kwenye simu janja inayotumika kukatia tiketi za mabasi ya masafa marefu, yaani mabasi ya kwenda mikoani. Kwa kutumia app hii utaweza kukata tiketi ya basi lolote kwenda mkoa wowote nchini Tanzania bila ya wewe kwenda ofisi husika ya kampuni hiyo kwaajili ya kukata tiketi.
Je App hii inamilikiwa na Nani?
App ya Tiketi Mtandao inamilikiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu (LATRA).
Nalipiaje Tiketi?
Kuna njia nyingi za kufanya malipo ya tiketi yako na baadhi ya njia hizo ni kulipa kwa kutumia huduma za malipo za mitandao ya simu kama M-Pesa kupitia namba 009009 au kufanya malipo kupitia akaunti yako ya benki.
Najuaje Kiasi Cha kulipia?
Kiasi cha kulipia huonyeshwa baada ya mtumiaji kujaza taarifa za safari yake kuwa anatoka wapi na anaenda wapi. Baada ya kufanya hivyo utaletewa orodha ya mabasi yaliyo na nafasi na yanayoelekea huko pamoja na gharama zake. Pia unaweza kuangalia makadirio ya nauli za mabasi ya mikoani zilizopangwa na LATRA hapa.

Naipakua wapi App ya Tiketi Mtandao?
App ya Tiketi Mtadao kwa sasa inapatikana PlayStore kwa hivyo watumiaji wote wa simu janja za Android wanaweza kuipakua na kutumia bila kupata shida yoyote ile. Pakua App hiyo hapa.
Mabasi yapi yanapatikana katika App hii?
Kuna makampuni mengi ya mabasi ambayo yameshajisajili katika mfumo huu ikiwemo kampuni ya Ester Luxury Coach, Kibomboi Royal Class na mengine mengi. Angalia Orodha Kamili hapa.
Maelezo ya ziada:
App hii imepakuliwa na zaidi ya watu 10,000
Ina ukubwa wa MB 4.0
Unaweza kuitumia kuanzia toleo la Android 4.1 na kuendelea.
Toleo lake la sasa ni Toleo namba 2.0.6
Iliwekwa PlayStore Machi 5, 2021.
No Comment! Be the first one.