Tanzania ni moja ya nchi nyingi tuu duniani ambazo wananchi wake wanatumia sarafu za kidijitali kufanya miamala mbalimbali kwa uhuru kabisa bila ya kuwepo maswali mengi lakini si kwamba mfumo huo umerasimishwa, la hasha!
Kwa miaka kadhaa sasa nchi, makampuni mbalimbali yanakubali kupokea malipo kwa sarafu za kidijitali mathalani Bitcoin, Ethereum na nyingine nyingi tuu lakini kwa Tanzania safari ya kurasimisha matumizi ya sarafu za kidijitali kufanya miamala mbalimbali bado ni ndefu.
Novemba 25 na 26 ya mwaka huu ulifanyika mkutano wa 20 wa taasisi za fedha nchini Tanzania ambapo kati ya mengi yaliyojadiliwa kwenye mkutano huo pia suala la sarafu za kidijitali lilizungumziwa. Inafahamika wazi Tanzania kama nchi imekuwa nzito kuhalalisha matumizi ya Bitcoin, Ethereum na sarafu nyinginezo kama njia mojawapo ya kufanya miamala.
Maneno ya Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga yanabainisha kuwa mambo bado hayajakaa sawa. Alisema kwa sababu tunajua sarafu za kidijitali si salama. Hatuwezi kusema ni muda gani itachukua kuleta miongozo, bado tunatafiti—tutatoa miongozo baada ya kumaliza utafiti wetu.
Hivyo, kwa maneno hayo kutoka kwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania ni dhahiri kuwa Watanzania waendelee kusubiri (safari bado ni ndefu) mpaka hapo wahusika watakapojiridha kuhalalisha matumizi ya sarafu za kidijitali.
Mgeni rasmi kwenye mkutano wa 20 wa taasisi za fedha alikuwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Chanzo: Benki Kuu ya Tanzania
No Comment! Be the first one.