Tovuti ni mkusanyiko wa kurasa zinazoelezea kuhusu kampuni, shirika au kutoa taarifa mbalimbali katika jamii. Kuna aina nyingi za tovuti ambazo unaweza ukasajili kwa ajili ya biashara au kampuni yako kama vile .com, .net, .tech, .tz na nyingine nyingi.
Wakati unafikiria kusajili tovuti ni muhimu sana kufikiria kwanza ni aina gani ya usajili wa tovuti ambayo inaendana na biashara au kampuni yako. Kwa hapa Tanzania kuna aina 12 tofauti za usajili wa tovuti kulingana na muongozo uliotolewa na TCRA. Muongozo huo unaonyesha aina za usajili pamoja na vigezo vya kusajilia kwa aina hiyo.
- .co.tz – Maalum kwa ajili ya tovuti za kampuni au biashara zilizosajiliwa Tanzania
- .or.tz – Maalum kwa ajili ya tovuti za mashirika yasiyo ya serikali
- .go.tz – Maalum kwa ajili ya tovuti za mashirika ya serikali ya Tanzania
- .ac.tz – Maalum kwa ajili ya tovuti za mashirika ya ki elimu
- .ne.tz – Maalum kwa ajili ya Matumizi ya mtandao au vifaa vya kimtandao
- .mil.tz – Maalum kwa ajili tovuti za jeshi la Tanzania
- .sc.tz – Maalum kwa ajili ya tovuti za shule za msingi na sekondari
- .me.tz – Maalum kwa ajili ya tovuti ya mtu binafsi au familia
- .hotel.tz – Maalum kwa ajili ya tovuti za hoteli
- .info.tz – Maalum kwa ajili ya tovuti za Habari
- .mobi.tz – Maalum kwa ajili ya tovuti za watoa huduma za simu
- .tv.tz – Maalum kwa ajili ya tovuti za stesheni za televisheni

Mpaka sasa tovuti zilizo sajiliwa kwa .tz zipo 22054 ambazo zimegawanyika kama ifuatavyo;
Jina | Idadi |
.co.tz | 18164 |
.or.tz | 1737 |
.ac.tz | 831 |
.go.tz | 770 |
.sc.tz | 207 |
.ne.tz | 51 |
.me.tz | 15 |
.hotel.tz | 7 |
.mil.tz | 6 |
.info.tz | 5 |
.mobi.tz | 5 |
.tv.tz | 5 |
Kuna jumla ya wasajili 62 wa tovuti za .tz na orodha kamili inapatikana hapa. Wasajili 10 bora wa tovuti za .tz ni hawa wafuatao.
Jina | Idadi ya Tovuti zilizosajiliwa |
Extreme web Technologies | 5670 |
Kilihost Limited | 3302 |
Route Africa Network Limited | 2514 |
DUDUMIZI TECHNOLOGIES | 2430 |
e-Government Authority | 878 |
Habari Node Ltd | 857 |
AFRIREGISTER | 829 |
Lexsynergy TZ Reg Limited | 712 |
Powercomputers Technology Ltd | 513 |
Itfarm | 372 |
No Comment! Be the first one.