fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Kompyuta simu Teknolojia

Coltan: Madini yanayotengeneza vifaa vya kielektroniki

Coltan: Madini yanayotengeneza vifaa vya kielektroniki
Spread the love

Coltan ni madini chuma yenye chembechembe za Niobium (Nb) na Tantalum (Ta). Columbite-tantalites maarufu kama coltan ni madini yenye umuhimu mkubwa sana katika utengenezaji wa vifaa vya kielektroniki kama simu janja.

Madini haya ya coltan huchimbwa kwa mkono na upatikanaji wake hautofautiani sana na uchimbaji wa dhahabu. 

Coltan ni moja kati ya madini adimu sana hapa duniani, yanapatikana katika nchi chache ikiwemo Democratic Republic of Congo (DRC), Australia, Canada, Brazil, China, Ethiopia na Mozambique. Congo ndio nchi inayoongoza duniani kwa usambazaji wa madini haya ya coltan ambayo hupitia Rwanda kuchakatwa na kuzitenganisha chembechembe za Niobium (Nb) na Tantalum (Ta) kwa ajili ya matumizi ya uzalishaji viwandani.

SOMA PIA  Facebook na Cambridge Analytica zaburuzwa mahakamani

Tantalum inayopatikana kwenye madini ya coltan hutumika kutengeneza vifaa vya ndani (tantalum capacitor) katika simu janja, kompyuta mpakato na kamera. Tantalum hutumika sana kwenye utengenezaji wa vifaa hivi vya kielektroniki kwa sababu zifuatazo:

  1. Ina uwezo mkubwa wa kupisha umeme
  2. Inaongeza hali ya sumaku
  3. Ina uwezo wa kuhimili joto kubwa
  4. Inatengeneza rangi mbalimbali katika kioo
  5. Inaongeza uwezo wa betri kutunza chaji

Madini haya hutumika pia katika utengenezaji wa ndege pamoja na baadhi ya mitambo yake kwasababu ya uwezo wake mkubwa wa kuhimili joto. Kutokana na kuwa na sifa nyingi madini haya yamechangia sana katika ukuaji wa teknolojia kwasababu yamerahisisha utengenezaji wa vifaa vidogo vya kielektroniki kama simu janja na kompyuta mpakato, yamechangia kuboresha spika na mic za vifaa vya kielektroniki pamoja na kuboresha uwezo wa lenzi zinazotumika kwenye kamera.

Je ulikuwa unafahamu kuhusu madini haya? Kama umefurahia makala hii basi endelea kutembelea tovuti yetu ili uendelee kujifunza mambo mbalimbali kuhusu teknolojia.  Soma makala zingine kuhusu teknolojia hapa.

Semu Msongole

Digital Marketing Strategist, Content Writer, and Social Media Manager at Teknokona Blog.

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania