fbpx
Teknolojia, Uchina

AliPay yaingia makubaliano na UEFA

alipay-yaingia-makubaliano-na-uefa

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Unapoona pameandikwa “Ali….” unanza kufikiri kuwa kitu hicho kitakuwa chini ya tajiri na bilionea Bw. Jack Ma. Na wala sio uwongo AliPay inamilikwa na mtu yuleyule mwenye Ailibaba.

Katika dunia la leo iliyotawaliwa na teknolojia miamala mingi inafanyika kielektroniki kwa sababu usalama pamoja na sababu nyinginezo. Lakini je, AliPay ni nini?

AliPay ni mfumo wa kufanya malipo kwa njia ya kidijitali ambao unawezesha kufanya miamala duniani ingawa kwa sasa ni Wachina wanaoishi Uchina au mtu mwenye akaunti ya benki ndio anaruhususiwa kufungua akaunti AliPay.

UEFA
Alipay-Mojawapo ya mifumo inayofanya malipo kwa kidijitali.

Makubaliano kati ya UEFA na Alipay.

Yapo makubaliano ambayo ambayo yamefikiwa kwamba Alipay kuweza kuwa njia mojawapo ya watu kufanya malipo ili kuingia viwanjani kuangalia mechi za UEFA kwa timu za taifa kuanzia mwaka 2018-2026 bila kusahau mashindano ya Euro 2020/24.

Hii ikimaanisha kwamba katika kiwanja ambacho mechi ya UEFA kwa timu za taifa inachezwa kwa siku hiyo mtu ataweza kulipia tiketi yake kwa njia ya Alipay kupata fursa ya kuingia kiwanjani kuangalia soka.

UEFA
Alipau kwenye ulingo wa kufanya miamala duniani.

Mpaka sasa AliPay ina wateja 700m huko Uchina wanaotumia mfumo huo wa malipo lakini suala zima la kampuni hiyo kuingia makubaliano na UEFA huenda namba ya watumiaji ikaongezeka mara dufu.

Vyanzo: Telegraph, Forbes

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  FAHAMU: Kampuni Ya HP kugawanyika!
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|