fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Kompyuta Microsoft Teknolojia Windows 11

Toleo la Windows 11 sasa ni rasmi; imetoka!

Toleo la Windows 11 sasa ni rasmi; imetoka!

Spread the love

Kwa miezi mingi zimekuwepo taarifa kuhusu toleo jipya la programu endeshi ambalo linamilikiwa na Microsoft kwa maana ya kwamba Windows 11 na hata kutolewa kwa watumiaji wachache lakini sasa inapatikana kwa watu wote; ni RASMI imetoka.

Leo hii Oktoba, 5 2021 Microsoft wameachia Windows 11 iweze kupatikana kwa watumiaji wote duniani kote ambapo kama kompyuta yako inakidhi vigezo basi utaweza kupata taarifa fupi kuhusu kuwezakupakua Windows 11. Sasa ukweli unabaki palepale kuwa si kompyuta zote zina sifa ya kutumia Windows 11.

Toleo la Windows 11

Toleo jipya la programu endeshi kwa upande wa Windows linapatikana bure (haihitaji malipo kuweza kupakua Windows 11).

Kuhama kutoka Windows 10 hadi 11

Windows 11 inaweza kuwekwa kwenye kompyuta kwa njia mbalimbali; mbali na kuipakua mara maraa baada ya kuona taarifa fupi kwenye sehemu ya kususha masasisho kuwa kompyuta husika inaweza kutumia toleo hilo la programu endeshi njia ya pili unaweza ukaishusha kutoka kwenye tovuti husika na kuiweka kwenye kifaa maalum kama memori ya ziada na kisha kukitumia kupakia Windows 11 kwenye kompyuta. Au ukashusha Windows 11 iliyo katika mfumo wa picha kutoka kwenye tovuti husika halafu ukaiweka kwenye memori ya nje mathalani diski (CD) kisha diski ikatumika kuweka programu endeshi kwenye kompyuta.

Toleo la Windows 11

Muonekano wa giza kwenye Windows 11.

Wapo ambao wanatumia ingizo hilo jipya kwenye kompyuta ilihali vifaa hivyo havina vigezo vya kuifanya programu hiyo endeshi kufanya kazi vyema hivyo hatushauri toleo hilo la programu endeshi kwenye kompyuta iwapo haijakidhi vigezo kwani kuna vitu itakuwa haipokei!.

Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania