Kutokana na ukuaji wa teknolojia ya mawasiliano serikali ya Tanzania imefanikiwa kutoa baadhi ya huduma zake kupitia mtandao. Huduma hizi za serikali zinazopatikana mtandaoni zimesaidia kuongeza ufanisi wa serikali kutoa huduma zake kwa wananchi. Mamlaka ya serikali mtandao (eGA) inahusika moja kwa moja na utengenezaji wa mifumo hii ikishirikiana na mashirika mengine ya serikali.
Huduma za serikali zinazopatikana Mtandaoni ni pamoja na:
Huduma ya Usajili wa Vizazi na Vifo kwa Njia ya Mtandao: Kupitia shirika la RITA serikali imefanikiwa kutoa huduma ya usajili wa cheti cha kuzaliwa pamoja na cheti cha kifo mtandaoni ambapo kwa kupitia huduma hii wananchi wameweza kuepuka usumbufu wa kuunga foleni katika ofisi za RITA na pia kuwawezesha wananchi kuhudumiwa kwa haraka zaidi. Huduma hii inapatikana hapa.
Huduma ya Mkopo kwa wanafunzi wa Elimi ya juu: Kupitia Bodi ya Mikopo HESLB serikali imefanikiwa kutengeneza mfumo wa uombaji wa mikopo kusaidia wanafunzi wanaoenda kusoma elimu ya juu. Mfumo huu umesaidia kuwapa nafasi wanafunzi waliopo sehemu mbalimbali Tanzania kutuma maombi yao ya mkopo kwa wakati. Tembelea tovuti hii kupata huduma hii.
Huduma ya Passport ya kusafiria: Serikali kupitia mamlaka ya Uhamiaji imetengeneza mfumo wa kutuma maombi ya kutengenezewa passport. Huduma hii imesaidia wananchi kuweza kuhudumiwa kwa haraka zaidi. Tembelea tovuti hii kupata huduma hii.
Huduma ya kutengeneza TIN Namba: Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato TRA imefanikiwa kutengeneza mfumo wa kutengeneza TIN namba kwaajili ya mtu binafsi na kwaajili ya biashara kwa njia ya Mtandao. Kupitia huduma hii wananchi wameweza kutengeneza TIN namba kwa haraka zaidi na kuendelea na shughuli zao za uzalishaji. Tembelea tovuti hii kupata huduma hii.
No Comment! Be the first one.