Shirika mama la mawasiliano na la kwanza nchini Tanzania kwa kifupi likifahamika kama TTCL limekuwa kwenye ulingo wa kupeleka huduma za simu na vitu vingine kwa zaidi ya miaka 50 na hadi leo bado lipo likiendelea kuwafikia wananchi.
Kama ulikuwa hujui basi fahamu leo kuwa hakuna kampuni yoyote inayokuja kutaka kufanya huduma za mawasiliano ya simu, intaneti bila kupitia TTCL na hivyo kulifanya kuwa ndio shirika mama nchini Tanzania. Hata hivyo, kwa miaka kadhaa TTCL ilikuwa haisikiki mpaka pale serikali ilipoamua kukaa nao chini na kutaka kufahamu wapi wasaidiwe. Matokeo yake tunayaona hadi leo.
Serikali ya Tanzania kupitia kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonaz amesema wataendelea kuwekeza fedha za kutosha kwa ajili ya shirika la mawasiliano Tanzania (TTCL) ili kufanikisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi wake popote walipo.
Siku zote mtu hujivunia na cha kwake na TTCL ndio shirika la mawasiliano ambalo serikali inalimiliki kwa asilimia kubwa tuu (kama si zote) lakini vilevile likiendeshwa na mzawa kwa maana ya Mtanzania, Bw. Waziri Kindamba. Mbali na serikali kuitegemea TTCL kuwapelekea wananchi huduma za mawasilino shirika hilo kupitia kwa wafanyakazi wake wametakiwa kufanya tafiti nyingi ambazo zitaleta matokeo chanya.
Hakuna mawasiliano bora bila ya umeme hivyo shirika hilo kupiti kwa Mkurugenzi wake mkuu, Bw. Waziri Kindamba amesema watashirikiana kwa karibu na Tanesco ili kuweza kupeleka huduma za mawasiliano kwa wananchi.
Chanzo: TBC
No Comment! Be the first one.