Twitter Na Vipengele Vipya, Ukijumuisha Na ‘Mixed-Media Tweets’!
Mixed-Media Tweets ni mfumo wa kutuma tweet ikiwa na picha na video katika Tweet moja hiyo hiyo.
Mixed-Media Tweets ni mfumo wa kutuma tweet ikiwa na picha na video katika Tweet moja hiyo hiyo.
Nadhani habari za Elon Musk kuhusu kuinunua Twitter ushazipitia zote hapa na ile nyingine hapa, tumeshajua kashainunua sasa kama kawaida kuna maboresho/mabadiliko inabidi yatokee.
Elon Musk afanikiwa kuinunua Twitter, jambo ambalo limeendelea kuleta mazungumzo mengi mtandaoni ya kuunga mkono au kupingwa na baadhi ya watumiaji wa mtandao huu maarufu.
Elon Musk ni moja ya watu maarufu zaidi duniani ambao wanamatumizi makubwa ya mtandao wa kijamii wa Twitter.
Twitter ni mtandao wa kijamii unaotumika na watu mbalimbali kubadilishana mawazo kupitia jumbe fupi. Mtandao huu wa kijamii ulianzishwa mwaka 2006, waanzilishi wakiwa ni Jack Dorsey, Biz Stone, Evan Williams na Noah Glass.
Mtandao wa kijamii wa Twitter kama ilivyo mingine mtu anaweza akatumia kupitia kivinjari kwa kutembela tovuti au kifaa chake cha kiganjani ambacho kinaweza kutoka kwenye programu endeshi mbili maarufu.
Twitter imekuwa ni miongoni mwa mitandao ya kijamii ambayo inafanyiwa maboresho ya mara kwa mara kutokana na sababu mbalimbali kitu ambacho kinaifanya kuwa ya kitofauti. Je, unafahamu kuhusu uwezo wa kutoa angalizo kuhusu chapisho?
Uwepo akaunti za uwongo kwenye mitandao ya kijamii ni suala ambalo linakera na sio zuri kwani watumiaji wake wanaathirika kwa namna moja au nyingine.
Kama ambavyo ilivyo mitandao ya kijamii mingi tuu kwamba unaweza kumtaja mtu kwenye kile ambacho umekiandika kwa maana ya wengine kuweza kuona vivyo hivyo kwenye Twitter inawezekana pia. Halikadhalika, hata kujiondoa kwenye mazungumzo inawezekana.
Twitter ina watumiaji wengi tuu ambao kwao ni mtandao wa kijamii muhimu sana kuzidi mingine. Umaarufu wake si mkubwa lakini umetokea kuwavutia watu mbalimbali ulimwenguni kote.
Twitter inapanua ufikiaji wa Hali yake ya Usalama kwa kuleta beta kwa takriban asilimia 50 ya akaunti nchini Marekani, Uingereza, Kanada, Australia, Ireland na New Zealand. Kampuni ilianza kujaribu kipengele hicho Septemba na idadi ndogo ya watu. Inapanua toleo la beta katika nchi za ziada zinazozungumza Kiingereza ili kupata maarifa zaidi na kutafuta njia za…
Mtandao wa kijamii wa Twitter unafahamika vyema kwa kuruhusu watu kuandika kitu kisichozidi idadi fulani ya maneno (pamoja na alama za uandishi) lakini hilo sasa huenda likabadilika na kuruhusu watu kuchapisha kitu katika urefu zaidi (kama makala).
Twitter imechukua hatua za kisheria dhidi ya sheria, inayoanza kutekelezwa nchini Ujerumani kuanzia Jumanne, ambayo inawalazimu makampuni ya mitandao ya kijamii kuzuia au kufuta maudhui ya uhalifu haraka na kuripoti makosa makubwa ya uhalifu kwa polisi, mahakama ya Ujerumani ilithibitisha Jumatatu.
Jack Sweeney, mwenye umri wa miaka 19 kutoka Florida, alikataa ofa ya $5,000 kutoka kwa Elon Musk ya kufuta akaunti yake ya Twitter inayofuatilia ndege binafsi ya bilionea huyo. ElonJet ina zaidi ya wafuasi 180,000 na hutumia roboti ambayo Sweeney alitengeneza kufuatilia safari za ndege za Musk, kisha hutuma kwenye twita lini na wapi ndege…
Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa Twitter Parag Agrawal anaendelea kurekebisha uongozi wa kampuni. Baada ya kuwaondoa wakuu wa uhandisi na usanifu mwezi uliopita, Agrawal analeta viongozi wapya wa timu ya usalama. Kampuni hiyo ilithibitisha kwa The New York Times kwamba mkuu wa zamani wa usalama Peiter Zatko ameondoka, huku afisa mkuu wa usalama Rinki Sethi ataondoka…
Serikali ya Nigeria imeondoa kusitishwa kwa shughuli za Twitter zaidi ya miezi sita baada ya kutangaza kwa mara ya kwanza kuzuiwa kwa kampuni hii kubwa ya mtandao wa kijamii nchini humo. Kashifu Inuwa Abdullahi, mkurugenzi mkuu na wakala wa teknolojia wa Nigeria, Wakala wa Kitaifa wa Maendeleo ya Teknolojia ya Habari (NITDA), alitoa tangazo hili…
Twitter, mtandao wa kijamii wenye wastani wa watumiaji milioni 206 kwa mwezi, umeripotiwa kufahamu na kupuuzia madhara ya huduma yao mpya ya Twitter Spaces inayowezesha watumiaji kufanya mazungumzo ya sauti ya moja kwa moja.
Kuna mengi tuu ambayo Twitter inapitia katika kipindi cha miezi kadhaa sasa kiasi kwamba hata aliyekuwa mtendaji mkuu wa kampuni hiyo, Bw. Jack Dorsey kuamua kujiweka pembeni na kazi hiyo lakini hatua hiyo imekuja na mabadiliko ya kutoruhusu usambazaji wa picha/video za watu binafsi bila ya ruhusa zinazowahusu!
Mwanzilishi mwenza wa Twitter Jack Dorsey anajiuzulu kama mtendaji mkuu wa kampuni. Nafasi yake itachukuliwa na afisa mkuu wa sasa wa ufundi, Parag Agrawal. Bw Dorsey, ambaye alianzisha Twitter mwaka 2006, amekuwa akihudumu kama mtendaji mkuu wa Twitter na kampuni ya malipo ya Square.
Moja ya mtandao wa kijamii ambayo haina watumiaji wengi duniani ni Twitter lakini imekuwa kwenye ushindani bila kusahau maboresho ambayo yanalengakuufanya kupata wateja wapya lakini kulinda kutopoteza ambao tayari wana akaunti.