Twitter ni moja kati ya mitandao mikubwa ya kijamii, licha ya kuwa mkubwa sana ni moja kati ya mtandao ambao unaaminika sana.
Kumbuka mtandao huo umenunuliwa na Elon Musk, yule tajiri namba moja kwa sasa. Ununuzi huo umepelekea kuwa kuwa na mabadiliko kadha wa kadha ambayo tumeyaandika >>HAPA<<
Kwa sasa moja kati ya badiliko ambalo linategemewa kufanyika ni kuondoa aina ya kifaa ambacho mtumijai wa mtandao amekitumia katika kuandaa tweet fulani.
Kingine ambacho mmiliki wa Twitter Bwana Elon Musk amekiongezea katika hili amesema hata hajui ni kwanini kipengele hicho kilikuwepo katika mtandao huo.
And we will finally stop adding what device a tweet was written on (waste of screen space & compute) below every tweet. Literally no one even knows why we did that …
— Elon Musk (@elonmusk) November 14, 2022
japokuwa baadhi ya wataamu waliamua kumjibu na kumpa faida ya kile kiashiria cha kuonyesha kuwa mtumiaji ame’tweet kutumia kifaa gani, bado na yeye alikuja na sababu kwanini sehemu hiyo iondolewe.
Kwa taarifa zilizopo ni kwamba uwezo wa utambuzi wa kifaa mtu anachotumia katika Tweet unachelesha App ya twiiter kufunguka kwa sekunde 2.

Kumbuka tangia bosi mpya wa Twitter apatikane kuna mabadiliko mengi hata watu kupoteza ajira zao na mabadiliko mengi ya kimtandao yametangazwa kufanyika na mengine tayari yameshafanyika.
Kingine kwa wale wanaotangaza makampuni kama vile ya simu zingine huko wao wanatumia simu zingine kwao itakua ni msaada mkubwa sana maana haitakua rahisi kwao kutangaza chapa nyingine huku akitumia chapa nyingine ku’tweet.
Ukaichana na haya yote ni kwamba mpaka sasa haijajulikana ni lini kipengele hichi kitaanza kufanya kazi rasmi

Kwa sasa ni kwamba boss wa Twitter bwana Elon Musk, ameandika dhamira hiyo katika ukurasa wake wa mtandao huo – ambao siku hizi ameonekana anautumia sana.
Ningependa kusikia kutoka kwako, naidnikie hapo chini katika uwanja wa maoni, je unadhini ni sawa tuu kwa mtandao huu kuondokana na hicho kipengele au ulibidi kibakizwe tuu?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.