Zipo simu za aina nyingi, zingine zina uwezo wa kuhimili uwepo wa maji kwa mda kadhaa [ water-resistant phone ] na zingine hazina uwezo huo [ Non water-resistant phone]
Kila simu iko tofauti kulingana na uundaji wake/mfumo wa simu hivyo yakupasa uwe makini sana pindi unakausha maji kwenye simu yako.
1: Non water-resistant phone
Hizi ni simu ambazo hazina uwezo wa kuhimili uwepo wa maji
Fanya yafuatayo endapo simu yako ya aina hii imeingia maji.
◾️Itoe simu yako kwenye maji haraka, kuendelea kuiacha simu kwenye maji ndio kuendelea kuiharibu zaidi.
◾️Zima simu yako haraka sana unaweza kutumia “power button” kuzima simu au unaweza kutoa battery ( Kama simu yako inaruhusu)
Kumbuka simu yako inatumia umeme, kuendelea kuwaka ilihali kuna maji kwenye circuit ni mbaya zaidi unaweza kuunguza vifaa.
◾️Kwa maji ya chumvi, beer na vimiminika vingine tumia kitambaa chenye unyevunyevu, ndiyo kwa sababu chumvi ni corrosive japo utaweka maji kwenye simu tena lakini itasaidia kuondoa chumvi na alcohol, simu nyingi zanasupport kitambaa chenye unyevu.
◾️Toa vitu kama sim-cards, micro-SD card na kama simu ina uwezo wa kutoa battery toa battery, kipindi unatoa hivyo vitu kuwa makini sana usitingishe simu yako maana unaweza kuingiza maji kwenye mifumo ya simu.
◾️Baada ya hapo kausha simu yako kwa kutumia kitambaa kikavu au Paper towel, kuwa makini usiweke maji sehemu zenye uwazi kama headphone Jack, charging port etc, safisha sehemu ulizotoa Sim cards, Micro-SD, na battery.
USIFANYE YAFUATAYO
◾️Usiweke kitambaa wala chochote kwenye charging port
◾️Usibonyeze key wala button yoyote kwenye simu yako.
◾️Usitingishe wala usigeuze gauze simu yako
◾️Usiweke karibu na feni au blower [ wengine mnajua hizi zinakausha maji lakini ni hatari ]
◾️Usijaribu ku-charge simu yako
◾️Usikaushe simu yako Kutumia vifaa kama hair dryers n.k[ external heat source]
BAADA YA HAPO
◾️Weka simu yako juu ya Kitambaa chepesi kikavu au taulo laini kisha weka sehemu ambayo ni kavu ila siyo juani subiri kwa siku moja au mbili [ recommend siku mbili ]
subiri simu yako ikauke na usiiguse kwa huo mda.
VIPI KUHUSU KUWEKA KWENYE MCHELE
Najua wengi mnajua na mmeambiwa kuwa njia nzuri ya kukausha simu iliyoingia maji ni kuweka kwenye mchele ambao haujapikwa, ambapo mchele utafyonza (absorb) unyevunyevu uliopo ndani ya simu ambao haukuweza kutoka pindi unakausha simu.
Hii theory huenda ikafanya kazi au isifanye kazi kutokana na aina ya simu, simu nyingi za kisasa hazifunguliwi kwa maana ya kutoa battery na zina sehemu chache zenye uwazi hivyo inakuwa ngumu kwa mchele kufikia sehemu zenye maji au kufyonza maji kwenye simu.
2: Water-resistance phone
Hizi ni simu zinazoweza kuhimili uwepo wa maji kwa mda kadhaa, lakini haimaanishi haziwezi kupata madhara endapo zimeingia maji.
Cha kufanya endapo simu yako [Water-resistant phone] imeingia maji
◾️Zima simu yako haraka
Hapa bado kuna mkanganyiko, Baadhi ya waundaji wa smartphone wanasema “hapana usizime” wengine wanasema “ndiyo zima”
Lakini kama una doubt/wasiwasi Basi unashauriwa kuzima simu, umenunua hela nyingi hiyo simu kwahiyo kinga ni bora zaidi.
◾️Kama ukiamua kuiacha simu yako ON
Usitumie accessories kama headphone wala usiicharge simu yako.
◾️Kwa maji ya chumvi, beer na vimiminika vingine
Safisha simu yako kwa maji safi sababu chumvi ni corrosive hivyo inaweza kuharibu simu ya aina yoyote iwe water resistant. Vimiminika vingine pia vinaweza kuleta madhara hivyo ni muhimu kuisafisha simu kwa maji safi au isoproply alcohol, lakini simu haiwezi kuhimili maji yanayo-tiririka kwa kasi inakupasa uisafishie kwenye ndoo au sink.
◾️Baada ya hapo ikaushe simu yako kwa kitambaa laini na kikavu.
Usiweke kitambaa au chochote kwenye charging port
Usitoe sim-card wala Micro-SD card
Usikaushe simu yako kwa kutumia vitu kama hair dryers etc
Baada ya kumaliza kukausha na kitambaa/taulo laini wekaka simu yako kwenye taulo laini kisha uiweke sehemu yenye uwazi au unaweza kutumia feni lakini isiwe na speed kubwa na isiwe karibu na simu.
Unaweza kuishika simu yako taratibu na kutikisa kidogo huku sehemu ya speaker ikiwa inaangalia chini.
Subiri simu yako ikauke ndipo uiwashe, haijalishi ni water resistance.
USHAURI
◾️Kama unataka kununua simu na budget yako inaruhusu ni vyema ukanunua “Water-resistance” au water proof phones
No Comment! Be the first one.