fbpx
Apple, IPhone, simu, Teknolojia

iPhone mpya kuzinduliwa Jumatano hii

iphone-mpya-kuzinduliwa-jumatano-hii
Sambaza

Kampuni ya Apple imetoa mwaliko kwa waandishi wa habari za teknolojia na wadau mbalimbali wa tasnia hiyo kuhudhuria tukio maalum katika ukumbi wa Steve Jobs Theater huko Cupertino, California siku ya Jumatano tarehe 12 Septemba 2018.

Siku hiyo inatarajiwa kuambatana na kutangazwa simu mpya za iPhone 9 na iPhone 11 au iPhone X Plus. Hata hivyo, majina ya simu hizo bado hayajathibitishwa kuwa ndio majina rasmi ila taarifa zinasema huenda zikazinduliwa simu tatu.

Tetesi zinasema kwamba iPhone X itakuwa na kioo cha ukubwa inchi 5.8, iPhone 11 itakuwa na inchi 6.5 na iPhone 9 inchi 6.1.

iPhone mpya
Muonekano unaotajwa wa iPhone X Plus

Pia bado haijajulikana sifa halisi ya simu zitakazozinduliwa ingawa kuna taarifa za tetesi kuhusiana na matoleo hayo mapya.

INAYOHUSIANA  Miwani janja toleo la pili kutoka Snapchat

Kwa taarifa kamili za uzinduzi huo na iPhone mpya endelea kufuatilia kwa karibu hapa teknokona ambapo utajua kila kinachoendelea katika masuala ya habari za teknolojia.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: , ,

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.