OnePlus kwa sasa ni kampuni ambayo inasifika vikubwa kwa simu janja zake ambazo zimeingia katika soko na kuwa ni mshindani mkubwa sana hata kwa makampuni makubwa.
Ni wazi kuwa imefanya vizuri sana katika soko la simu janja na kwa sasa inajiaandaa dhahiri kuingia katika soko la tabiti ikifika mwaka 2023.
Kwa taarifa ambazo hazipo rasmi sana inasemekana kwamba tabiti hizo zitajulikana kama OnePlus Pad na pia inasemekana zitakuja na kuhakikisha kuwa zinashindana vikali na zile kutoka katika kampuni ya Apple (iPad).
Lakini kingine ambacho inabdi kifahamike ni kwamba ukiachana na kampuni kuongeza tabiti, ni kwamba ina simu janja, Tv na vifaa vingine vya kuvaa kama vile saa janja n.k.
OnePlus has a tablet in development.
Launch is scheduled for next year! #OnePlusPad— Max Jambor (@MaxJmb) November 14, 2022
Ni wazi kwamba katika soko la tabiti hakuna ushindani mkubwa ukifananisha na masoko mengine kama vile katika soko la simu janja.
Hii kwao ni faida maana kama bidhaa ikiwa ni nzuri hawatatumia nguvu kubwa sana katika kahakikisha kua wanaliteka soko.
Kama ni mfuatiliaji mzuri sana wa OnePlus utagundua kuwa ilisemekana tabiti ya kwanza kabisa kutoka katika kampuni hiyo itatoka mwaka 2022 lakini mwaka tunaumaliza huku ikiwa haijafika sokono.
Kingine ni kwamba inasemekana tabiti hiyo itakuja na sifa hizi
- Kamera ya 13MP na 5MP ambazo zote ziko nyuma na huku kamera ya mbele ikiwa ni 8MP kwa ajili ya picha za selfi.
- Uwezo wa betri ni 10,090mAh ikiwa na uwezo wa kajaza chaji kwa haraka (fast charging).
Hizi zikiwa ni baadhi ya sifa ambazo zinadhaniwa zitakua katika tabiti hiyo ambayo itatoka mwakani japokua hatuna uhakika nazo dhahiri.
Ni wazi kwa teknolojia ambayo OnePlus wanayo tabiti hii itakuja kuleta chachu katika soko nasi hatuna budi kuisubiria kwa hamu tabiti hii
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chinii katika eneo la comment, je unadhani tabiti hiyo italeta ushindani katika soko?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.