fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

OnePlus OnePlus Oppo Oppo simu Smartphones

Tuuelewe Vizuri Muunganiko Wa Oppo Na OnePlus!

Tuuelewe Vizuri Muunganiko Wa Oppo Na OnePlus!

Spread the love

CEO wa OnePlus bwana  Pete Lau alisema kuwa OnePlus na Oppo kwa pamoja makumpuni hayo mawili yanakua pamoja bega kwa bega ili kuhakikisha kwamba yanaleta bidhaa nzuri sokoni.

Sasa ikishakua hivi unaweza ukajiuliza nani ni nani hapa? maana makampuni yote mawili yanafanya kazi na kuzalisha bidhaa zinazofanana karibia asilimia mia.

Hapa kwa kwamba OnePlus inakua ni brand ya Oppo (na kuwa chini ya Oppo). Ifahamike kuwa Oppo nayo ipo chini ya kampuni ambayo inajulikana kama BBK Electronics.

Mkurugenzi Na Mwanzilishi Wa OnePlus Bwana Pete Lau

Kama bado hujaelewa ni kwamba iko hivi BBK Electronics > Oppo > OnePlus. Kingine amnacho kimeelezwa ni kwamba bado kampuni hizo mbili zinaweza kufanya mambo yanayojitegemea.

Katika muunganiko huo, Bwana Lau ambaye ndio/alikua mkuu wa OnePlus  moja kwa moja ndiye atakae kuwa mkuu kabisa wa kitengo cha bidhaa (uzalishaji).

SOMA PIA  Tarehe ya uzinduzi wa simu janja OnePlus Nord 2 5G yafahamika!

Ni wazi kuwa brand hizo zitafanya kazi kwa kujitegemea kila moja lakini vile vile kumbuka kampuni mama ambayo ni BBK Electronics bado inamiliki brand kubwa kama vile Vivo na RealMe.

Naweza kusema kuwa brand za OnePlus na Oppo kulingana na muunganiko huu ni kwamba zitzweza kupata malighafi kwa haraka zaidi ili kuhakikisha kawa zinakuja na bidhaa nzuri zaidi katika soko.

CEO Wa Oppo Bwana,Tony Chen

CEO Wa Oppo Bwana,Tony Chen

Bado kuna tetesi kuwa bado uhusiano huu haujawekwa hadharani kwa baadhi ya vitu. Bado haipo wazi sana kwa makampuni yote mawili kwamba yatakuwa yanajihusisha na nini kwa mwenzake.

SOMA PIA  Google wakamilisha kuwanunua wahandisi 2,000 wa HTC

Ningependa kusikia kutoka kwako, Niandikie hapo chini katika eneo la comment, Hii umeipokeaje? je unahisi muungano huo utakua na tija kweli na utaleta mapunduzi katika soko?

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania