Kwenye vifaa vingi vya kielektroniki ambavyo tunatumia huwa vinakusanya baadhi ya taarifa zetu sio? Lakini kingine kizuri mara nyingi huwa hazikusanywi mpaka vifaa hivyo vituombe ruhusa, moja ya kifaa hicho ni simu ya iPhone kutoka Apple.
Kuna sehemu huwa inauliza ila App fulani iweze kufuatilia baadhi ya taarifa zako, na wewe mtumiaji unaweza ukaamua kuruhusu jambo hilo au ukalikataa katika baadhi ya vifaa vya Apple.
Kwa taarifa ambazo zimetoka hivi karibuni ni kwamba ukatae au ukubali kwa taarifa zako kufuatiliwa bado taarifa zako zitafuatiliwa tuu.
Katika utafiti ambao umefanywa katika soko la App Store, Apple Music, Apple TV, Books na baadhi ya App zinazomilikiwa na kampuni ya Apple umeonyesha dhahiri kuwa taarifa zinakusanywa hata kwa zile App ambazo watu hawajaruhusu.
Vitu ambavyo vinaangaliwa/vinakusanywa ni kama vile ni aina gani ya matangazo ambayo mtu anaangalia na mengine mengi tuu na bado ripoti inasema hili linafanyika hata kama ukiwa umezima ile sehemu ya “iPhone Analytics”.
Shitaka ambalo lipo na linaikabili kampuni ni lile la kukiuka ulinzi wa taarifa za watu (usalama/ulinzi wa taarifa za watumiaji).
Kitu ambacho kinaonyesha dhahiri kwamba kesi hii ni kubwa sana ni kawa sababu moja kati ya sifa ya Apple ni uwezo wake wa kulinda taarifa za watumiaji wake na hii imkeua ni ushindi kwa wapinzani wake.
Kama ukienda katika Settings > Privacy & Security > Analytics & Improvements kwa watumiaji wa iPhone hapo utakua na uwezo wa kuruhusu au kukataza taarifa hizo kufuatiliwa, lakini kwa repoti iliyotoka inasema kuwa taarifa hizo zinakusanywa hata ukikataza.
Wao Apple wanasema kama ukiruhusu taarifa hizo wazikusanye basi watakusanya kwa lengo la kuboresha vifaa vyao (iPhone) na kusaidia katika kuboresha mfumo mzima na hata kutatua matatizo mbalimbali.
Watafiti wengi kutoka katika maeno mbalimbali wamekuja na jibu hilo (kukusanya taarifa) baada ya kufanya uchunguzi wa kina.
Kuna kupindi tuliandika kuw Apple mbioni kuleta matagazo katika sehemu za Apple Store, iBook na sehemu zingine. Sasa tunapata taarifa kwamba baadhi ya taarifa ambazo zinakusanywa na kampuni ni kuangalia mteja anaangalia matangazo ya aina gani katika App Store?
Hili peke yake tuu linaweza likawa linaibua maswali mengi sana sio? Lakini hatuna budi kusubiri na kuona kesi hii itaendelea vipi.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je wewe unaona kesi hii ina mashiko au ni mbwembwe tuu?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.