Moja kati ya simu ambazo zimejipatia umaarufu mkubwa sana katika soko la simu janja ni simu za iPhone na zina matoleo mengi.
Mara kwa mara simu za iPhone zimekua zikishikilia namba za juu kama moja ya simu bora mara kadhaa kwa mwaka huku Samsung akiwa ndio mshindani wake mkubwa.
Kwa fununu ambazo zipo ni kwamba simu hiyo itatoka mwaka 2024 na simu hizo zitakua na kioo cha ukubwa wa inchi 6.2 hadi inchi 6.3 na hii ni kwa toleo la iPhone 16 Pro Max.
Hiki ni kioo kikubwa sana maana kwa sasa ukilinganisha na kioo cha iPhone 14 Pro Max ambacho kina inchi 6.7 na hata iPhone 15 Pro Max itakua na ukubwa huo huo.
Kingine ni kwamba itakua nyembamba sana ukilinganisha na matoleo ambayo tayari yapo ya Pro Max.
Pande wake wa picha utakua na maboresho makubwa sana haswa haswa kwa upande wa mwanga, settings za kamera hiyo na muonekano katika picha husika.
Kumbuka na kwa mwaka huu iPhone 15 Pro Max itakuja na lensi ya Periscope ambayo itakau na uwezo mkubwa sana wa kuvuta (zoom) mbali sana.
Simu hizi zimetoka mbali sana na zilikua zina umbo dogo ambalo lilikua likiruhusu kuwa na kioo kidogo, kumbuka kulikua mpaka na iPhone yeye kioo cha inchi 3.5 na hapo ni mpaka iPhone 5 ilivyotoka na ilikua na kioo cha inchi 4.
Kwa haraka haraka fikiria vioo vya simu vitakuja kuwa ni vikubwa kiasi gani? Maana ukitaka uso wa kioo mkubwa si kuna tabiti? Au ni mapema kusema inatosha?
Niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je hii umeichukiliaje? Je unadhani ni utaweza kutumia matoleo haya pindi yakitoka tuu? Ningependa kusikia kutoka kwako.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
No Comment! Be the first one.