fbpx

Ijue Spark 2 simu mpya kutoka Tecno

0

Sambaza

TECNO Mobile imeendelea kuimarisha msimamo wake kama bidhaa namba moja kwa simu rununu katika soko la Afrika kwa kuzindua simu mpya nyingine ya Spark 2 hivi karibuni.

Simu hii ambayo inakuwa ni toleo la pili la familia ya Spark imezinduliwa katika hoteli ya Sheraton katika jiji wa Lagos, Nigeria na ina mfumo endeshi ambao haujaenesa kwenye simu janja nyingi.

Spark 2 inakuja na ukubwa wa kioo cha inchi 6 chenye teknolojia ya HD na simu yenye wembamba mzuri itakayomrahisishia mtumiaji kuishika kwa urahisi na wepesi.

simu mpya kutoka Tecno

Spark 2 ni simu itakayokidhi mahitaji ya wateja wao kwa kuwa simu yenye ufanisi na itakayopatikana kwa bei ndogo itakayomuwezesha kila mtu kumudu kuinunua.

Upande wa kamera Spark 2 inakuja na kamera nyepesi kuliko Spark iliyotangulia. Kamera ya mbele ina 8MP na ya nyuma 13MP. Kamera zote zitatoa picha nzuri kwa kuwa zitakuwa na uwezo wa kuingiza mwanga zaidi hata katika mazingira ya mwanga hafifu.

INAYOHUSIANA  Kiwanda cha kutengeneza simu kuanzishwa nchini Rwanda

Spark 2 itatumia Android 8.1 Oreo (Go Edition) ambayo imeboreshwa zaidi na kuwa nyepesi kwa watumiaji itakuwa na RAM ya 1GB pamoja uhifadhi wa ndani wa 16GB.

Kwa upande wa Betri itakuwa na ujazo wa 3500mAh ambapo unakadiriwa kudumu na chaji kwa saa 24 ya kuzungumza. Kadhalika, simu hii inakuja na teknolojia ya ulinzi ya kutambua sura Face ID vilevile alama ya kutumia kidole. Hili bila shaka litawafurahisha wapenzi wa Tecno Spark 2.

simu mpya kutoka Tecno

Tecno Spark 2 itapatikana katika rangi za ajabu za Nyekundu, Nyeusi, Dhahabu, Bluu na Bordeaux. Tayari imeshaanza kuuzwa madukani kote nchini.

Sifa nyinginezo za Spark 2

Jukwaa

Prosesa:                   MediaTek MT6580WP
Kasi ya Prosesa:    Quad-Core 1.3GHz

INAYOHUSIANA  Hizi hapa namba zinazotumika kwa utapeli wa mtandaoni

Uhifadhi

Memori ya ziada:   Unaweza kuweka mpaka ukubwa wa mpaka  32GB

Mawasiliano

Teknolojia:                  GSM / WCDMA / LTE
Kadi za simu:             Laini mbili

Bei ya simu hii kwa sasa ni Tsh. 280,000. Kwenye maduka mbalimbali inawezekana ikawa nadra sana kupatikana kutokana kwamba haina muda mredu tangu kuzinduliwa kwake.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.