fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Motorola simu Teknolojia

Leo hii tuifahamu simu janja Motorola Edge 20

Leo hii tuifahamu simu janja Motorola Edge 20

Spread the love

Mwezi Julai mwaka huu ulikuwa na ingizo jipya la simu janja kutoka Motorola ambao wameendelea kuja na rununu ambazo zinaendana na kile ambacho wateja wanahitaji sokoni. Motorola Edge 20 ilikuwa ni moja ya simu janja ambayo ilikuwa na habari lukuki za chini kwa chini.

Makampuni mengi siku hizi yanaweka ubunifu, nguvu nyingi kwenye vitu ambavyo vitaiuza rununu kwa haraka mara tu pale itakapoonekana. Motorola Edge 20 ni moja ya simu hizo ambapo imewekwa nguvu nyingi kuanzia kwenye ubunifu wa muundo wake mpaka kwenye kamera. Fuatana nami kuweza kufahamu undani wake:

SOMA PIA  Jumla ya masaa bilioni 1 ya video hutazamwa YouTube kila siku!

Kamera|Muonekano

Kwa muonekano ni simu janja nyembamba isiyochukua nafasi kubwa na si nzito. Kwenye kamera ile kuu ina MP 108, inayofuatia ni MP 8 ambayo unaweza kukuza kitu mara 3 zaidi na ya mwisho imewekwa MP 16 bila kusahau taa 2 za kuongeza mwanga sehemu hafifu.

Motorola Edge 20

Mpangilio wa kamera za nyuma kwenye Motorola Edge 20. Kamera ya mbele ina uwezo wa kurekodi picha mnato za ubora wa, 4K na 1080px.

Kioo|Memori

HIi simu ina kioo chenye urefu wa inchi 6.7 cha ubora wake ni OLED pamoja na kamera ya mbele iliyowekwa chini ya kioo lakini katika mtindo wa kufanya mbele kuwepo kwa shimo dogo na ina MP 32. Upande wa memori simu hii ina GB 8 za RAM, 128 GB au 256 GB-diski uhifadhi.

Motorola Edge 20

Inawezekana kwa mtumiaji kuchagua kiasi cha ung’avu wa vitu vinavyoonekana kwenye simu. Kamera ya mbele ina uwezo wa kurekodi picha mnato za ubora wa 1080px.

Betri|Mengineyo

Betri lake lina 4000mAh, 30W za teknolojia ya kuchaji haraka, inatumia USB-C 2.0. Ni simu janja yenye teknolojia ya 5G, kipuri mama ni Qualcomm Snapdragon 778G 5G, teknolojia ya kutumia alama ya kidole imewekwa kwenye kitufe cha kuzima/kuwasha simu, inatumia Android 11 lakini ipo kwenye mpango wa kuweza kuhamia hadi Android 13.

Motorola Edge 20

Motorola Edge haina sehemu ya kuchomeka spika za masikoni, redio wala mahali pa kuweka memori ya ziada. Ina WiFi, Bluetooth 5.2, NFC, inatumia kadi mbili za simu, inalindwa na kioo cha Gorilla 3 upande wa mbele na nyuma ni plastiki.

Gharama yake inaanzia $593.99|zaidi ya Tsh. 1,366,177 kwa bei ya ughaibuni na tayari imeshaingia sokoni rangi zake ni Kahawia, Nyeupe, Bluu.

Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania