Umewahi kujiuliza kuna umuhimu wa kufanya updates za simu yako au upotezee tuu? Makala tunakuelezea baadhi faida muhimu kwa wewe kuhakikisha simu yako inapata masasisho (updates) yote muhimu kwa wakati.
1. Masasisho (Updates) yanaongeza ulinzi
Kwenye simu yako unaweza kua na taarifa zako binafsi kama akaunti za benki, nywila, vyeti vyako nk ukiwa umevihifadhi kwenye simu yako. Wadukuzi kila siku huja na njia mpya na ‘malwares'(teknolojia za udukuzi) mpya za kudukua taarifa za watu kwenye simu zao, ndio maana hata kampuni za simu nazo huja na masasisho ya mara kwa mara ili kuisaidia simu ijilinde na aina yeyote ya kirusi kipya kwa muda huo.
Kila wanapotoa masasisho yenye sifa za kuboresha usalama inakuwa ni kwa ajili ya kushinda teknolojia mpya za udukuzi au kupambambana na kirusi kipya cha kiteknolojia ambacho kinasambaa mtandaoni, wanaziba madhaifu yaliyopo kwenye mfumo unaotumiwa na simu.
2. Kulinda vifaa vinginevyo
Kutokufanya updates mara kwa mara hupelekea urahisi kwa wadukuzi (hackers) kuweza kudukua mfumo endeshaji wa kifaa chako, na baada ya kudukuliwa pengine wanaweza kupata pia data zako muhimu kama vile nywila, barua pepe na namba za simu za kuwawezesha kudukua akaunti zako au vifaa vyako vingine. Kumbuka, wakiwa na data zako muhimu inakua rahisi kuingilia na hivo vifaa vingine pia ambavyo vinatumia taarifa sawa na za kwenye simu yako.
3. Mambo Mapya (Features)
Kitu kingine kwenye kukubali masasisho (updates) kwenye simu yako ni pamoja na kuwezesha vitu vipya (features) ambazo zimeongezwa kuboresha muonekano wa programu endeshi (OS) pamoja na kuwezesha mambo/teknolojia mpya kwenye simu yako: mfano kwa sasa kuna iOS 16.1.1 na android 13 zote hizo zina mwonekano wa tofauti na unaovutia kabisa ukilinganisha na matoleo ya nyumba..
Kuruhusu masasisho kunaongeza hata utendaji kazi mzuri wa simu yako.
Je kuna madhara yoyote kukubali updates mapema?
Katika kukubali masasisho ya simu yako, hakikisha unayapa muda kidogo. Hapa namaanisha angalau siku 3 – 4, ili kama masasisho haya yanaleta tatizo basi watengenezaji simu wanakuwa tayari washatoa sasisho la ziada la kuhakikisha kifaa kisiathirike kiutendaji kutokana na sasisho kuu.
No Comment! Be the first one.