Wajapani ni noma. Matumizi ya teknolojia yanaweza kweli kutumika kwa kitu chochote wakati wowote katika ulimwengu wa leo. Kama mtu anayeishi katika Jiji la Dar es Salaam au pande za visiwani, itabidi kukubali kuwa kupata vazi lenye uwezo wa kupunguza joto la msimu flani si kitu kibaya.
Kwa hili wajapani waja na suruali hewa-baridi maarufu kama Air-Condition (AC). Wanaamini uingizaji hewa nzuri ya kiubaridi katika suruali yangu pale kwenye joto, kutaweza kuweka viungo vingi viwe poaaa, hahahahaha. Na zaidi ya yote suruari hizo zinakuja na shati zake kabisa.
Kampuni itengenezayo nguo hizi inaitwa Kuchofuku, je wewe utanunua nguo ya namna hii ikija madukani?
Hayo ndo mambo ya teknolojia! 😉
No Comment! Be the first one.