fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Amazon Intaneti Teknolojia

Fahamu kuhusu kampuni ya Amazon na Huduma zake

Fahamu kuhusu kampuni ya Amazon na Huduma zake
Spread the love

Amazon ni kampuni ya teknolojia ya kimataifa iliyopo Marekani ambayo inajihusisha na biashara za mtandaoni, huduma za mtandaoni pamoja na akili bandia (Artificial Intelligence). Kampuni ya Amazon ni moja kati ya kampuni kubwa 5 za teknolojia ya mawasiliano zilizopo nchini marekani ambazo ni Google, Meta, Microsoft na Apple.

Kampuni ya Amazon ilianzishwa mwaka 1994 na mmiliki wake Jeff Bezos ambapo ilianza kwa kutoa huduma ya kuuza na kununua vitabu mtandaoni kupitia tovuti yake ya amazon.com. Baada ya kufanikiwa kutoa vizuri huduma hiyo tovuti hiyo iliongeza nakuwezesha watu kuuza na kununua vifaa vya kielektroniki, magemu na samani kwa rejareja.

kampuni ya Amazon

Mizigo inayosafirishwa na Amazon

Huduma zinazotolewa na kampuni ya Amazon ni pamoja na:

SOMA PIA  WhatsApp yaleta status zenye mtindo wa Snapchat, Facebook waendelea kuiba vizuri!

Amazon Prime: Ni huduma inayopatikana kwa njia ya usajili wa kulipia Amazon, Huduma hii inapatikana katika nchi mbalimbali na huwezesha watumiaji kupata huduma za ziada au huduma zinazopatikana kwa malipo kwa wateja wengine wa Amazon. Huduma hizo ni kama kuagiza na kupata bidhaa ndani ya siku moja au mbili, kusikiliza mziki na vitabu vya kielektroniki, kuangalia video mtandaoni na huduma zingine za manunuzi ya bidhaa.

SOMA PIA  Kadi janja kwa ajili ya Usafiri wa Mabasi ya Mwendo Kasi zaanza Kuuzwa

Amazon Kindle: Ni kifaa cha kielektroniki cha usomaji, Kifaa hiki kimetengenezwa na Amazon. Amazon Kindle huwawezesha watumiaji kuvinjari, kununua, kupakua na kusoma vitabu vya kielektroniki, magazeti, majarida na vyombo vingine vya habari vya kidijitali kupitia mitandao.

Pia Amazon hutoa huduma mbalimbali maalum kwaajili ya matumizi ya kibiashara au kampuni kama Amazon Business na Amazon AWS.  Amazon Business ni huduma ya kujisalili inayotolewa na Amazon ambayo inasaidia biashara mbalimbali na makampuni kununua bidhaa kwa matumizi ya kiofisi kwa bei nafuu pamoja na kupata ofa mbalimbali za punguzo la bei pamoja na kutolipishwa hela ya kusafirisha mzigo.

SOMA PIA  Simu janja ya kwanza yenye "V" mbili

Amazon AWS ni huduma za kimtandao zinazotolewa na Amazon kama uhifadhi wa taarifa za kampuni mtandaoni. Huduma hii inaweza kutumiwa na biashara kubwa, makampuni pamoja na serikali za nchi mbalimbali.

Hizi ni baadhi tu ya huduma zinazotolewa na Amazon lakini zipo nyingine nyingi. Endelea kutembelea tuvuti yetu uweze kujifunza zaidi kuhusu teknolojia na matumizi yake. Soma makala zetu zingine hapa.

Semu Msongole

Digital Marketing Strategist, Content Writer, and Social Media Manager at Teknokona Blog.

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania