fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Dell HP Kompyuta Tablet

Kampuni Ya Lenovo Yakaribia Kushika Soko la Kompyuta!

Spread the love

Kwa wengi wetu tutakapowaza kununua kompyuta mara moja tunawaza HP, Samsung au Dell, na mara chache Acer, ila je unajua Lenovo namba mbili duniani kwa mauzo ya kompyuta, tena ndani ya wiki chache zijazo kampuni hii inatemewa kushika namba moja!

Lenovo ikifanikiwa itakuwa ndiyo kwa mara ya kwanza kwa kampuni ya Kichina kushika namba moja katika vifaa cya elektroniki, na haishangazi kwani takribani nusu ya mauzo ya kompyuta za Lenovo yanafanyika nchini Uchina.

Takwimu za soko zilizotoka zinazoelezea hali ya soko la kompyuta, zinaonesha bado  Hewlett-Packard (HP), bado ndiyo kampuni kubwa duniani katika uuzaji wa komyuta, ikiwa mbele ya kampuni zingine lakini ikiwa inafuatiwa kwa mwendo kasi wa Lenovo.

Makampuni ya kusoma masoko ya Gartner na IDC, yote mawili siku ya leo yalitoa makadirio yao ya soko. Ingawa wao hupima soko tofauti, wote wawili wameonyesha pengo kati ya HP na Lenovo kuzidi kuwa dogo katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

Kwa ujumla, Gartner imesema, watu binafsi na makampuni yalinunua kompyuta 87,470,000 katika kipindi cha miezi ya nne hadi sita, ambazo ni sawa na kuporomoka kutoka 87,600,000 katika kipindi kama hicho cha mwaka uliopita. HP imewazidi wachuuzi wengine wote, kwa kuuza mashine 13,040,000 na kuchukua asilimia 14.9 ya sehemu ya soko la duniani kote. Lenovo, kulingana na makadirio ya Gartner, ilipitwa kidogo tuu, iliuza mashine 12,820,000, ambayo ni jumla ya asilimia 14.7 ya soko, na mauzo haya yamevunja rekodi kwa ukuaji wa takribani 15 kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Ukuaji unaona na wengi unachangiwa na muenendo wa kampuni ya Lenovo kuuza kompyuta zake kwa faida ndogo sana kulinganisha na wapinzani wake, Dell na HP. Mauzo ya HP na Dell yameporomoka kwa takribani asilimia 12 kwa kila mmoja katika kipindi cha mwaka mmoja. Hivyo kwa mwenendo huu inategemewa Lenovo itaweza kushika namba mmoja muda wowote sasa, inategemewa baada ya kipindi cha miezi mitatu repoti nyingine ya mauzo itakapotoka itathibitisha hili.
SOMA PIA  Windows 10 Kuuzwa katika USB - Flash Disks

Chart: Top 5 Worldwide PC Vendors, Market Share (unit shipments)Description: Source: IDC Worldwide Quarterly PC Tracker, July 11, 2012Note: IDC’s Worldwide Quarterly PC Tracker provides PC market data for over 80 countries by vendor, form factor, brand, processor brand and speed, sales channel and user segment. The research includes historical and forecast trend analysis as well as price band and installed base data.For more information, or to subscribe to the research, please contact Kathy Nagamine at 1-650-350-6423 or knagamine@idc.com.Further detail about this tracker can be found at:http://www.idc.com/tracker/showproductinfo.jsp?prod_id=1Tags: Q2 2012 PC data, 2Q12, 2012Q2, Desktop, Notebook, PCAuthor: IDCcharts powered by iCharts

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania