Kampuni kongwe katika huduma za intaneti ya Yahoo imepata janga baada ya wajanja wa masuala ya mtandao kuweza ku’hack’ moja ya huduma ya Yahoo iitwayo Yahoo Voices.
Wamefanikiwa kuiba anuani za barua pepe 435000 na maneno yake ya siri (Passwords), kuamkia leo Alhamisi.
Hii imekuwa aibu kubwa kwa kampuni ya Yahoo na kwa namna moja inaharibu sura ya kampuni kwa wateja wake. Kwa sasa kampuni hiyo inawasihi wateja wake wafanye mabadiliko ya maneno ya siri kwenye akaunti zao.
Shambulizi hili lilifanywa na kikundi kinachojiita D33D Company, na baada ya kupata data hizo waliziweka kwenye mitandao mbalimbali.
Watu Hao (Hackers) Walitangaza Mafanikio Kupitia Twitter |
Tovuti wa Yahoo Voices ni mtandao wa kijamii unaowawezesha watu kuweka picha, makala na vitu vingine kwa ajili ya jamii nzima ya wana’Yahoo Voices’.
Kama unataka kuwa na uhakika kama Anuani yako imenusurika unaweza kutembelea mtandao huu http://dazzlepod.com/yahoo/ ambapo kuna orodha ya barua pepe zote zilizoathirika.
Yahoo Wamesema Wanachunguza Jambo Hili |
Mitandao mingi inajikuta katika wakati mgumu sana kutokana na mashumbulizi ya aina hii mara kwa mara huku wanaofanya vitendo hivi wakidai wanawasaidia watu na makampuni kutambua ni jinsi gani masuala ya ulinzi wa data muhimu yasivyopewa kipaumbele.
Kampuni ya Yahoo inasema inachunguza ni vipi jambo hili lilitokea.
No Comment! Be the first one.