Linapokuja suala la mitandao gani ya simu imejiwekeza vizuri linapokuja katika suala la ‘Social Media management’ kwa lugha yetu uendeshaji na ushiriki katika mitandao ya kijamii naiweka Tigo namba moja.
Kuendesha akaunti za mitandao ya kijamii inaitaji timu nzuri sana, kwani haitakiwi iendeshe kimalengo ya matangazo tuu kwani utawachosha wateja wako hivyo inahitaji ubunifu wa hali ya juu ili kuongeza mazungumzo na wateja wako. Na hichi ndo kitu ambacho timu ya Tigo inafanya.
Leo kupitia ukurasa wao wa Facebook wameanzisha shindano linalohusisha timu yake ya Masoko (Marketing) katika pambano la kupunguza unene likesema ‘Kitambi: Hakitakiwi Challenge’. Kuna kurusa za makampuni pinzani huwa zimepoa sana, activity ipo ziro nje ya matangazo ya kibiashara tuu na malalamiko na maswali kutoka kwa wateja yasiyojibiwa, TeknoKona tunaipa Tigo tano za nguvu kwa ubunifu walionao!
Picha za wafanyakazi wa Tigo wanaohusika na masuala ya masoko zitakuwa zinawekwa kwenye ukurasa wa Facebook kila jumatano, na wapenzi wa Tigo wanatakiwa kuwapa ‘Like’ wale wanaoona wanaongoza katika kufanya mabadiliko ya kupunguza mwili, ‘unene’.
Tunategemea hii itakuwa ‘challenge’ kubwa na kuleta chachu kwa makampuni mengine katika kuboresha timu zao za kuendesha akaunti zao za mitandao ya kijamii.
No Comment! Be the first one.