fbpx

Tweet ya Lukas Podolski wa Arsenal yalipua Bomu Twitter

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Leo nilitazama video moja iliyokuwa ni mahujiano ya kwanza rasmi kufanyika kwa Bwana David Moyes tokea atimuliwe kazi ya umeneja wa timu ya Manchester United. Siandiki kuhusu mpira ila ni kuhusu kitu muhimu sana alichokisema juu ya ukuaji wa teknolojia ya mawasaliano hasa hasa kwenye suala la mitandao ya kijamii. Alidai kwa miaka ile ya nyuma wapenzi wa timu hawakuwa wanauwezo wa kutoa shutuma nyingi kwa uzito haraka sana kiasi cha kulazimisha mabadiliko ya haraka pale wasipofurahisha kama siku hizi, kwani kwa sasa kupitia mitandao kama Facebook na Twitter timu hizi zinapata presha kubwa kutoka kwa wapenzi pale timu isipokuwa inafanya vizuri. Na kabla siku haijaisha, Podolski kupitia akaunti yake ya Twitter ameweza kuzima uzushi wa yeye kuuzwa hapo Januari mwakani kwenda timu pinzani ya Tottenham.

pod2

Podolski alijibu akisema ‘Jehenamu ya Arsenal itakauka kwa barafu kabla ya uhamisho huu kafanyika‘ akaongezea msisitizo kwa kutumia hashtagi/alama-reli za kuonesha yeye ni Arsenal damu.

INAYOHUSIANA  Gari la Umeme Kutoka Faraday Future ni Kama Gari la Kuendeshwa na 'Batman'

Wataalamu wengi walishatabiri teknolojia ya mawasiliano na ujio wa mitandao ya kijamii inayoraisisha taarifa kutoka na kusambaa kwa haraka utaleta mabadiliko kweli kweli….na yanaonekana kwa sasa. Hii ni moja ya tweet maarufu zaidi kwa siku ya leo, na tunategemea itashika rekodi katika tweet maarufu zaidi labda kwa mwaka huu pia.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply