fbpx

Spotify na app mpya kwa ajili ya Apple

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Kama unapenda kusikiliza muziki mtandaoni na ni mkereketwa wa teknolojia bila shaka utakuwa unafahamu huduma ambayo Spotify wanatoa kupitia intaneti.

Kampuni hiyo (Spotify) wameamua kutoa app mpya kabisa kwa ajili ya saa janja za Apple ambapo wahusika wameweka huko ili kuwavutia watumiaji kulingana na sifa ilizonazo:

Uwezo wa kuunganisha programu tunishi husika na spika au kifaa cha kidijiti. Imeelezwa kuwa programu hiyo inahusiha maboresho wa jinsi muziki unavyotoka hivyo kufanya mtu kupata ladha ladha inayovutia kwa kile anachosikiliza.

Uwezo wa kucheza kitu kilichoshuwa kutoka mtandaoni (Podcast). Mbali na kuwa na uezo wa kucheza muziki kupitia mtandaoni pia programu tumishi husika inao uwezo wa kucheza miziki/picha jongefu zilizoshushwa kutoka mtandaoni.

programu tumishi mpya

Programu tumishi inaruhusu kurudisha kwa sekunde kumi na tano kuweza kusikiliza kile ambacho hukukisikia vizuri au kilikupita.

Uwezo wa kusikiliza musiki bila kutumia intaneti. Programu tumishi mpya ya Spotify imeahidi kuboreshwa kwa toleo litakalofuata mabapo mtumiaji ataweza kupata huduma bila ya kuwa hewani, yaani kuunganisha intaneti ili mtu aweze kupata kile ambacho programu inaweza kufanya.

INAYOHUSIANA  Baada ya siku na miezi kadhaa Apps za HTC zarudi Google PlayStore

Ili kupata programu tumishi husika ni lazima uwe unatumia  Spotify (v.8.4.79) uliyoshusha kutoka kwenye soko la programu tumishi (Apple Store).

Vyanzo: Tech Crunch, The Verge

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.