Katika teknolojia ya karibuni makampuni mbalimbali yanafanya shughuli ya utengnezaji wa simu wamekuwa wakiongezea nakshi naksi kwa kuweka sehemu ndogo ya umbo la herufi “V” kwenye kioo.
Katika hali ambayo ni ya utofauti wa aina yake kampuni moja ya simu ina simu janja ambayo ina “V” sehemu mbili tofauti na tulivyokwishazoea kuona rununu ikiwa na kitu hicho sehemu moja tu.
Rununu Sharp Aquos R2 mbali na kuwa na sifa ya kipekee lakini pia ina kioo kirefu kwa inchi kadhaa ingawa kuzidiwa urefu/upana na mtangulizi wake.
Urefu/upana sio kigezo kioo cha simu kutokuwa kipana, kitu cha msingi ni ubunifu.
>Kioo+Kipuri mama.
Kioo cha kwenye simu husika kina ung’avu ambao nyuma ya pazia unabebwa na IGZO LCD 1080 x 2280px (inchi 5.2) lakini pia kioo ni kigumu kupasuka kutokana na teknolojia ya Gorilla Glass 3. Upande wa kipuri mama imewekwa Snapdragon 845.
>Kamera.
Kipengele ambacho ni kivutio cha wengi katika miaka ya karibuni. Ni vyema ukafahamu kuwa Sharp Aquos R2 ina kamera moja mbele yenye MP 8 na nyingine upande wa nyuma ikiwa na MP 22.6.
Sharp Aquos R2 simu ya kwanza kabisa kuwa na umbo la herufi “V” upande wa juu na chini kwenye kioo.
>RAM+Diski uhifadhi.
Simu hii haina toleo tofauti touti kwa maana ya kwamba kuwa na RAM/memori ya ndani tofauti nyingine bali imewekwa nafasi ya GB 64-diski uhifadhi na GB 4 za RAM lakini pia ukiwa na uwezo wa kuweka memori ya ziada ya mpaka GB 512.
Hakuna haja ya kusubiri masasisho ya Android 9 Pie kwani simu hiyo imewekwa moja kwa moja toleo hilo. Betri yake ina 2500mAh. Vilevile, inatumia teknolojia ya USB Type C kupeleka chaji kwenye simu.
Rangi na mengineyo.
Simu husika ipo katika rangi tatu; Kijani, Nyeupe na Nyeusi. Pia inatumia teknolojia ya IP68 kuzuia maji kuingia kwenye simu, ina sehemu ya kuchomeka spika za masikioni.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|