fbpx

Mwanzilishi wa WhatsApp awasihi watu wafute akaunti Facebook

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Mmoja kati ya waanzilishi wa huduma ya WhatsApp awasihi watu wafute akaunti Facebook. Bwana Brian Acton ameyasema hayo wiki chache zilizopita alipokuwa anashiriki mdahalo katika chuo kikuu cha Stanford nchini Marekani.

Bwana Brian aliwaambia wanafunzi wa chuo hicho ya kwamba kufuta akaunti ya Facebook linaweza likawa ndio jambo jema zaidi la kufanya kwa sasa ili kujilinda na matumizi mabaya ya data zao.

watu wafute akaunti Facebook

Tweet ya Brian Acton: Muda ni sasa, #futaFacebook

Brian aliacha kazi Facebook 2017 baada ya kutofautiana na uongozi wa juu wa Facebook kuhusu kuanzishwa kwa huduma za kibiashara katika app ya WhatsApp hasa hasa zinazohusisha data za watumiaji wa app ya WhatsApp. Inasemakana katika makubaliano yao ya mwanzoni ya kuuza app hiyo kwa Facebook walipewa ahadi ya kwamba Facebook hawatakuja kutaka kufanya jambo kama hili katika huduma ya WhatsApp.

waanzilishi whatsapp

Waanzilishi wa WhatsApp, Brian Acton na Jan Koum wote wameacha kazi kutokana na kutofautiana na Facebook

Hii si mara ya kwanza kwa Brian kuhimiza watu wafute akaunti Facebook. Anaona kwa sababu za kibiashara Facebook wataweza kuruhusu utumiaji mbaya wa data za watumiaji wa app ya WhatsApp.

Inasemekana muda si mrefu watumiaji wanaweza jikuta wanapata matangazo katika eneo la kuangalia ‘Status’ za marafiki zao.

Vipi je una mtazamo gani na uamuzi wa Facebook kuleta mambo ya kibiashara katika app ya WhatsApp?

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Baada ya iPhone 6 Plus, Apple kuja na iPad Pro
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.