Kuna namna nyingi za kushusha video kwa kutumia simu na kompyuta ila inaleta furaha sana ukijua njia rahisi na bure ya kupata burudani kama tubeMate – programu ya bure ya android ya kushusha video kutoka youtube, facebook, vimeo, dailymotion na tovuti nyingine.
Urahisi wa tubeMate unakuja kwenye uwezo wa kushusha video ukiwa pale pale tubeMate. Hamna haja ya kufungua programu nyingine.
Kwenye tubeMate, unaweza kuitafuta video kirahisi kwa kutumia alama ya kutafuta – > . Baada ya hapo, utaishusha kwa kutumia alama ya kijani itakayojitokeza upande wa juu kulia. Utachagua ukubwa wa video unaotaka kushusha. Kwa simu yenye uwezo wa kawaida, tumia 426X240(MP4) na chini ya hapo, ila kama una simu yenye uwezo mkubwa kama Samsung S4, basi una uhuru wa kuchagua ukubwa wowote. Mwishoni mwa orodha hiyo, unaweza pia kushusha video yoyte kama mwimbo wa kawaida (AUDIO MP3). Ukimaliza kufanya uchaguzi sahihi, utaona video yako ikishuka kwenye eneo la taarifa la simu yako.
Ingawa tubeMate ni mahsusi kwa kushusha video, unaweza pia kuangalia video humo humo, kutengeneza ‘playlist’ zako mwenyewe na kushirikisha watu wengine nyimbo na programu yenyewe.
Programu hii haipatikani kwenye ‘Playstore’, ila kama programu nyingine zinazokinzana na taratibu na kanuni za Google, unaweza kuipata kwenye tovuti mbalimbali kwenye mtandao, nyingine zikiwa salama na nyingine za hatari! Teknokona inakupa tahadhari kuwa mwangalifu na programu unazozipata nje ya masoko maalumu ya programu. Unaweza kuipata tubeMate kupitia tovuti hii hapa.
Kwa hali ya kawaida, huwezi kupakia programu yoyote isiyotoka ‘ Google Playstore’ kabla ya kubadilisha chaguzo za usalama. Kuiruhusu tubeMate kupakia, inabdi kubadilisha mpangilio wa usalama kwa kuingia ‘settings’ > security na kwenye ‘Unknown sources’ ruhusu kwa kuweka tiki.
Umeionaje programu hii? Una maoni, maswali, habari na ujanja zaidi? Ungana nasi kupitia teknokonatz@gmail.com na pia kwenye kurasa zetu za facebook na twitter.
No Comment! Be the first one.