Si muda mrefu tangu tuandike kuhusu vitumizi (apps) kama Evernote na OneNote zinazotumika kunakili na kuhakikisha haupotezi kumbukumbu muhimu. Google Keep ni moja ya hizo app tulizotaja ambayo ni rahisi kutumia, yenye sifa nzuri na ina mvuto wa kipekee. App hiyo sasa inakuwezesha kunakili kwa kuchora na kuutuma mchoro wako kirahisi!
Google wameongeza kipengele cha kuchora ambacho kinakupa uhuru wa kuchora kwenye kurasa tupu au juu ya picha uichaguayo kutoka kwenye app nyingine kama Gallery. Unaweza kukianzisha kipengele hicho kipya kwa kutumia widget mpya na zilizoboreshwa za Keep kwa kubonyeza kitufe chenye alama ya peni. Kama umefungua app tayari, unaweza pia kuona hicho kitufe chini kabisa, kwenye kuandika nakala mpya. Katika ukurasa wa kuchora, unaweza kutumia rangi mbalimbali, unaweza kukata ka-eneo ulikochora na ku-kahamishahaisha na kufanya utundu mrahisi.
Kwa nini ushushe toleo hili?
Google wanaendelea kuonesha umahiri wao wa kutengeneza app zenye mvuto, zinazokidhi mahitaji ya wengi, huku zikibaki kuwa rahisi kutumia. Kipengele hiki kipya si jambo kubwa ila litakupa ahueni pale unapohitaji kunakili namba haraka kwenye matumizi ya kawaida au kumtumia mwenzako ka-mchoro ka-kufurahisha kwani ni rahisi sana kuisambaza michoro yako baada ya kuitengeneza, tofauti na app zingine.
Mbali na maboresho ya Google Keep, Evernote nao wameongeza widget mpya za kurahisisha matumizi ya app yao. Tuambie kama umejaribu kipengele hizi vipya na unatumiaje app gani ya kunakili uipendayo, kwenye mazungumzo hapo chini.
One Comment