Sasa unaweza kuona mbuga ya wanyama ya Gombe bila ya wewe mwenyewe kuenda Kigoma.
Hii ni baada ya kampuni kubwa ya kiteknolojia ya Google kuungana na taasisi ya utafiti ya Dr. Jane Goodall na kutengeneza taswira za uhalisia wa ndani ya hifadhi ya Gombe ambayo inaweza kupatikana popote duniani, wakati wowote kwa intaneti.
Mbuga ya Kitanzania ya Gombe ni maarufu duniani kwa nyani na sokwe ambao Dr. Jane Goodall, mtafiti anayeheshimika duniani na raia wa uingereza anayekaa Tanzania, amekuwa akiwachunguza kwa zaidi ya miaka 54. Wanyama hao ambao imegundulika kwamba wana tabia zinazoendana sana na za binadamu (wakiwa na asilima 98 ya chembe chembe za uhai zinazofanana na za binadamu) iko katika wilaya ya Kigoma, mkoani Kigoma.
Kwenye makala ya Jumanne kwenye blogi ya Google, Google imeeleza kwamba walitumia mabegi ya mgongoni yaliwekewa kamera maalumu zinazoitwa ‘Street View Trekkers’ kupata maelfu ya picha za nyuzi 360 kutoka njia nyembamba za hifadhi ya Gombe. Picha hizo ni zikiwemo picha ya Ziwa Tanganyika na nyumbani kwa Dr. Goodall, ya nyani wakiwa ufukweni, pamoja na ya sokwe, akiwemo mmoja anayeitwa ‘Google!’ wakiwa mapumzikoni. Pamoja na taswira hizo, imeelezwa kwamba Google wametayarisha waraka unaoelezea hali ya maeneo yanayoizunguka Gombe yaliyoathiriwa na kuangushwa kwa misitu.
Akielezea suala la kufanikisha teknolojia ya Street View kuingia Gombe, Lilian Pintea, Raisi mwandamizi wa taasisi ya Jane Goodall amesema kuwa Street View ni kifaa kipya kinachowawezesha watafiti kufuatilia na kushirikisha dunia kuhusu kinachoendelea na tabia za sokwe kwenye maskani yao ya msituni. Itasaidia pia jamii ya wanamisitu inayotumia teknolojia za mkononi kwa kuwapa rekodi za kihistoria ambazo kila mtu anaweza kuelewa na kutumia. Taswira za Street View zitatumika pia katika kufundishia pamoja na kuwa kifaa cha tafiti.
Kuweza kujionea mwenyewe taswira za Gombe kupitia Google Maps na Street View, bofya linki hii.
Picha na:
No Comment! Be the first one.