fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Maujanja simu Teknolojia

Kosa Kubwa Linalofanyika Katika Kutengeneza ‘Password’ Za Simu Janja Na Tablet!

Kosa Kubwa Linalofanyika Katika Kutengeneza ‘Password’ Za Simu Janja Na Tablet!

Spread the love

Kama hutaki mwizi au ukipoteza simu yako mtu aweze kupekenyua vitu vyako, unahitaji kuwekea kifaa chako loki ambayo italinda hasa hasa zile data zako za muhimu.

Loki zipo za aina nyingi sana siku hizi –Asante kwa kukuwa kwa teknolojia – kuna zile za kutumia kidole, ‘pattern’ na hata zile za kuweka namba na maneno kama kawaida.

Kwa mfano watumiaji wengi wa simu za android wamezoea ‘pattern’ (ile loki ya kuunganisha vile vidoti doti). Sasa ni makosa gani yanafanyika katika kuweka loki vifaa vyetu?

Hapa tunafeli sehemu moja, wengi wanaotaka kuweka loki katika vifaa vyao wanapenda kuweka loki rahisi ambayo wataweza hata wao kuikumbuka mara moja tuu. Lakini kumbuka sio vizuri kuweka loki rahisi kwani ni rahisi sana watu kuotea loki hiyo.

Kwa mfano nenosiri kama “0000,” “1111,” “1234” au “0852 (kucheza na vibonyezo vya kati),”  sio za kuzitegemea kabisa kwani ni rahisi sana mtu kuziotea.

Lakini unaweza sema kuwa sababu watu hawapendi kuwa na nenosiri  refu sana ni kwamba linatesa kila mara kuliandika wakati unatumia simu yako. Fikiria kwa siku unaangalia simu yako mara ngapi? Sasa pata picha kila mda huo unakuwa unaandika nenosiri ambalo ni refu sana.

SOMA PIA  Hillary Clinton akamata fursa ktk gemu la Pokémon Go

Nadhani kutokana na  jambo hili ndio maana watengenezaji wa simu janja na tablet wameamua kuja na njia rahisi kabisa kama vile kwa kutumia sense za vidole, kwa kutumia uso na ‘Pattern’ (maarufu katika simu za Android).

Kwa watu wengi kuchora Pattern ni njia wanayoipenda zaidi kwani ni rahisi sana kuiingiza na pia ni rahisi kwa vichwa vyetu kuikumbuka mara moja. Pia kwa sababu kuna pointi 9 inazobidi uziunganishe hivyo inafanya kuwe na aina nyingi ambazo mtumiaji anaweza seti neno siri lake.

TATIZO KUHUSU PATTERN

Katika auchunguzi uliofanywa na aliyekuwa mwanafunzi wa chuo cha Norwegian University of Science and Technology, Marte Løge, alibaini kuwa kati ya ‘pattern’ 4000 asilimia 77 walikuwa wanaanza kuchora kuanzia katika moja kati ya kona nne za juu kabisa. Asilimia 40 walianza katika kona ya juu upande wa kushoto kabisa.

Kwa haraka haraka watu wengi huwa wanaanza kuchora ‘pattern’ zao na kwa kupitia katika vinundu vine tuu mpaka vitano saa zingine. Kwa kufanya hivyo wanashusha ule ugumu wa kuweza kutoa loki hizo. Sawa kwa mtu kukisia bado ni vigumu lakini kwa watu ambao wamebobea katika kazi hizo, wadukukuzi (hackers) wanaweza wakawa wamerahisishiwa kazi kwa kiasi flani.

Usipende Kuweka 'Pattern' Za Namna Hii password

Usipende Kuweka ‘Pattern’ Za Namna Hii

Katika ‘Pattern’ kuweka shepu za herufi kama vile “L” au “Z” kuanzia katika kona ya kushoto ya juu ni rahisi sana kwa mtu kuotea kwani zinajulikana sana. Pia watu wanafeli pale wanapoweka refu hizo kutoka kwa majina yao au kutoka kwa watu wao wa karibu.

SOMA PIA  Samsung njiani kufungua viwanda zaidi nchini Marekani

Nadhani kama tunakubaliana kuwa kama unatumia aina hizo za ‘Pattern’ ni rahisi sana mtu kuiotea na akafanikiwa kutoa loki katika kifaa chako. Sasa ni njia gani za kufanya kuhakikisha kuwa unakuwa na ‘Pattern’ ambayo sio rahisi kwa mtu kuiotea?.

TENGENEZA PATTERN NGUMU

Kitu cha kwanza kabisa cha kufanya ni kwamba tengeneza ‘pattern’ ambayo itahusisha vile vinundu 8 au 9. Mdukuzi au hata mtu anaekupekua ni vigumu sana kuotea ile yenye vinundu 8 mpaka 9 kwa sababu mara nyingi watu wanatumia vinne mpaka vitano.

Hata kwa kutumia vinundu vingi, kumbuka usitumie vinundu hivyo katika kutengeneza ‘pattern’ yenye umbo la herufi kwani itakua nib ado rahisi kuikisia. Cha kufanya hapa anza kuchora ‘pattern’ hiyo kwa kuanzia vinundu vya kati

SOMA PIA  Kwa mara nyingine walio na iPhone 12 na 12 Pro kutengenezewa bure

Kwa mfano angalia hii (lakini usitumie hii kama ilivyo)

Mfano Wa Kuigwa (haha!)

Mfano Wa Kuigwa (haha!)

Itakuwa ni vigumu kwa mtu kuweza kuiotea hii sio? Hata saa nyingine mtu akikuona kabisa unaiandika hii bado inaweza ikawa ni vigumu kwa yeye kuikumbuka.

ONGEZA ULINZI ZAIDI

Kwa kawaida ukiwa unachora pattern yako kuna kimstari kinaonyesha ulipoanzia kuchora mpaka unapoishia. Hii ni sawa tuu na kuonyesha neno siri lako tuu wakati unaliandika (show password). Ni nzuri kwa kukusaidia kuepuka kukosea wakati wa kuchora lakini kumbuka watu walio karibu na wewe na wao wanaweza wakaona

Cha kufanya katika kifaa chako chako cha Android nenda katika Settings>>Security and uncheck “Make pattern visible.” Ili kubadilisha. Katika vifaa vingine unaweza ukakuta katika Settings>>Lock Screen. Hapa sasa kwa mtu ambae ana nia ya kukuangalia atashangaa tuu vidole vinapita haraka katika vinundu kwa haraka na bila shaka atashindwa kukariri.

Mpaka sasa natumai na wew ni mtaalmau wa kutengeneza pattern sio? Tuandikie sehemu ya comment kama njia hii imekusaidia. Tembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona kwa habari za kiteknolojia kila siku. Kumbuka TeknoKona Daiima Tupo Nawe katika Teknolojia!.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Comments

  1. […] 2. Makosa katika utengenezaji wa password za Simu na […]

  2. […] Ufunguaji wa simu wakati ikiwa imelokiwa ulikua ni rahisi sana hapo mwanzo, lakini kumbuka kuwa ilikua ni rahisi vile vile kuweza kuibiwa taarifa zako kwani mtu angeweza kufungua kifaa chako kwa urahisi. […]

TeknoKona Teknolojia Tanzania