fbpx

simu, Teknolojia

Japan ‘Kuishiwa’ Namba Za Simu! :-)

japan-kuiishiwa-namba-za-simu

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Sambaza

Hivi namba za simu zinaweza kuisha kweli? Japan kuishiwa namba za simu za kuweza kutumika na hivyo wamekuja na mfumo mpya wa kuweza kutengeneza namba za simu nyingine zaidi.

Namba mpya zinazokuja zitakuwa ndefu zaidi (tarakimu 14) kuliko zile za nyuma (tarakimu 11). Namba hizo mpya zinatarajiwa kuwa tayari na kuanza kutumika pindi ifikapo mwanzoni mwa 2021 hiyo ni kwa sababu namba ambazo zinatumika sasa zinatarajiwa kuisha ifikapo 2122.

SOMA PIA  Mambo 10 Ya Kushangaza Unayoweza Fanya Ukiwa Google!

Mitandao mikubwa ya nchi hiyo imeshakubaliana na hili wazo la kutengeneza namba zingine za simu. Mitandao kama NTT Docomo, KDDI, na  SoftBank imejadiliana kuwa kwa kuanzia waje na namba bilioni 10 (za tarakimu 14).

Japan kuishiwa namba
Japan kuishiwa namba: Ukurasa Wa Kupigia Simu

Teknolojia ya 5G inategemea kuanza kutumika rasmi Japan ifikapo mwaka 2020 hivyo ni wazi kwamba utumiaji wa laini katika vifaa vya intanet utaongezeka kwa kiasi kikubwa sana na ukifutatilia vizuri jambo hili ndio linalofanya kwa kiasi kikubwa kuwe kuna uhitaji mkubwa wa namba zingine.

SOMA PIA  Simu za 2019: Hizi ndio simu 10 zilizouzika zaidi mwaka 2019

Makubaliano ya kuja na mfumo mpya wa namba za simu za Japan ili kuwezesha laini bilioni moja zingine umehusisha mazungumzo ya vyombo vya serikali na wadau wengine wote muhimu – hii ikiwa ni pamoja na mitandao ya huduma za simu.

SOMA PIA  Simu za iPhone 6, SE, X hazitatengenzwa tena

Lakini tatizo hili sio la kwanza kuikumba Japan tuu hata UK kuna kipindi waliongea namba kwa baadhi ya maeneo baada ya wa watumiaji wa maeneo hayo kuishiwa na namba za simu.

Niandikie mawazo yako hapo chini sehemu ya maoni na karibu tena TeknoKona kwa habari za kiteknolojia. Kumbuka daima tupo nawe katika teknolojia na sayansi.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Sambaza

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com