fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Mtandao wa Kijamii

Twitter: Herufi 140 Zinatosha Kabisa, Hakuna Nyongeza!

Twitter: Herufi 140 Zinatosha Kabisa, Hakuna Nyongeza!

Spread the love

Kama ulikua unategemea Twitter iongeze idadi ya maneno katika Tweets, ondoa wazo hilo kwani hilo halitawezekana tena

Hapo awali Twitter walitoa ripoti kuwa wanafikiria kuongeza idadi ya maneno katika Tweets watu watakazokuwa wanatuma. Namba ambayo ilifikiwa ni kwamba kampuni ilikua inafikiria kuifanya tweet moja iwe hadi na herufi  10,000 (ni herufi nyingi sana kwa Twitter niliyoizoea)

Mwisho Wa Tweet Ni Herufi 140 Tuu twitter

Mwisho Wa Tweet Ni Herufi 140 Tuu

Mkurugenzi wa mtandao huo wa kijamii Bw. Jack Dorsey ametoa taarifa hizi ijumaa iliyopita (18/03/2016) kuwa Mtandao huo hauna mpango tena wa kuongeza idadi ya maneno katika Tweets zitakazo kuwa zinatumwa.

Kumbuka umaarufu wa idadi chache ya maneno katika Twitter (herufi 140) ndio umechangia kwa kiasi kikubwa kuzaliwa kwa vifupi vingi vya maneno kama vile OOMF,FF na vingine vingine. Maneno yakiwa mengi kwa mtazamo wangu Twitter inaweza  ikapoteza utamu wake (kama unanielewa)

Kwa wengine hii inaweza ikawa si habari njema kwako kwa wanapata shida kutuma Twitter nyingi wakielezea kitu kimoja. Wengine katika kujielezea kwa ufupi hawawezi na idadi kubwa ya herufi zingewasaidia. Mpaka leo kuna watu wanaandika Tweets zaidi ya moja katika kuelezea kitu kimoja tuu.

SOMA PIA  Watendaji Muhimu Wanne waondoka Twitter

Hata hivyo kuna ujanja ujanja mwingine wa kutumia katika kuhakikisha unavuka herufi 140 katika Tweet. Kwa mfano unaweza ukapandisha picha katika Twitter na ukabofya sehemu ya “Who’s in this photo” ili kuwa ‘tag’ wale ambao wapo katika picha hiyo. Sasa badala ya kufanya hivyo unaweza ukaamua kuongeza maneno mengi tuu ambayo ulitaka kuandika ila herufi zikawa hazitoshi.

Jack Dorsey

Jack Dorsey

Japokuwa hii ilitupambaza wengi kwa kujua kuwa mabadiliko yatakuja. Lakini Bw. Dorsey amesema tusahau kabisa katika mabadiliko hayo na pia amesema Twitter moja kati ya malengo yake ni kuwasaidia watumiaji wake kutuma Tweet ili kuweka mawasiliano ya haraka haraka.

SOMA PIA  Facebook Wameficha Gemu la Chess katika app ya Messenger

Baada ya hayo kusemwa, tuandikie sehemu ya comment nini maono yako juu yanhili. Tembelea TeknoKona kila siku. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania