Twitter jana Jumanne ilipata tatizo la kimtandao ambalo ni kubwa kutokea kwa ndani ya miaka kumi, tatizo hilo liliwaathiri watumiaji wengi kuanzia saa nne asubui hadi mida ya saa kumi na moja jioni katika siku ya jumanne.
Taarifa kutoka katika mtandao huo inasema kwamba tatizo hili lilitokana na wao kubadilisha code ya ndani na baada ya kugundua hilo wakaondoa mabadiliko hayo na hii ikarudisha huduma katika hali ya kawaida.
Japokuwa kumekuwa na matukio machache ya kimtandao kwa mtandao huu miaka ya karibuni ila tukio la mwaka 2008 linakumbukwa baada mtandao huu kuzidiwa na watumiaji wake wakati wa tukio la apple. Pia mwaka 2014 itakumbukwa kwamba mtandao huu ulipotea walau kwa dakika 45 na hii ndiyo ili kuwa mara ya mwisho mtandao huu kupata matatizo kama haya.
Some users are currently experiencing problems accessing Twittr. We are aware of the issue and are working towards a resolution.
— Twitter Support (@Support) January 19, 2016
Hii ni Tweet ya akaunti ya msaada ya mtandao huo ikionesha kuwa wanashughulikia tatizo
Tatizo la jana liliwakumba watumiaji wote ingawa waliolalamika hasa walitoka katika kundi la wanaotumia mtandao huu kupitia mtandao ila pia watumiaji wa Android na iOS wapo waliolalamika.
No Comment! Be the first one.