Wateja wa Tigo ambao wanajiunga na vifurushi vya mwezi ama wiki kuanzia wiki iliyopita wanapata huduma ya Whatsapp kwa bure.
Huduma hii ambayo ni kwa wateja wenye simu zenye uwezo wa intaneti inatolewa na mtandao huu ili kuonesha dhumuni la Mtandao wa Tigo katika kuchochea maisha ya kidigitali na pia kuongoza katika kuleta teknolojia na ubunifu katika jamii.
Ili uweze kutumia huduma hii unachotakiwa kufanya ni kuhakiksha unajiunga na kifurushi chochote kutoka TiGo cha mwezi ama cha wiki ambacho kinapatikana katika menyu yao ya vifurushi inayopatikana kwa kubonyeza *148*00#. Huduma hii inapatikana katiak simu za iPhone Blackberry, simu zote za Android na pia simu za Nokia Symbian 60 phones.
Huduma hii inamaana kwamba sasa watumiaji wa TiGo na ambao wanajiunga vifurushi vya wiki ama vya mwezi hawata kuwa na mawazo juu ya vifurushi vya intanet ili kutumia whatsapp, wao wataweza kuitumia whatsapp vile wanapenda bila hofu ya kumaliza data zao. Ila kumbuka kwamba huduma hii itakufanya utumie whatsapp tu sio Instagram ama Facebook ambazo pia ni app zinapendwa.
Utumiaji wa WhatsApp hautakuwa unatumia intaneti ya bando lako
Wanachofanya TiGo ni kuhakikisha kwamba kila mteja anayetumia kifurushi cha wiki ama cha mwezi anaendelea kupata data ambazo zinahusiana na Whatsapp hata kama data yake imeisha kwa maana kwamba kama ulijiunga kifuruchi cha wiki ambacho kina kupa mb 500 na umekwisha zimaliza basi hutaweza kutumia huduma nyingine za internet ila Whatsapp itakuwepo.
Mitandao yote mikubwa hapa Afrika mashariki ipo katika mashindano ya kupata watumiaji wengi zaidi na wakudumu, na njia pekee ya kuwakamata watu wengi ni kuwapa huduma za kiutofauti na hii ikiwa ni pamoja na promosheni mbalimbali. Vodacom ya Tanzania imezindua kampeni yake ya ongea deilee huduma ambayo inampa mtu dakika za kuongea bure kila siku wakati Airtel wao wapo na kampeni yao ya Mkwanjika ambayo inatoa nafasi ya kushinda hadi shilingi milioni mia tatu kwa kukwangua vocha yako.
Kwa Tanzania pekee Whatsapp inawatumiaji karibu milioni nane katika watumiji takribani bilioni moja duniani kote. Mtandao huu uliwaliruhusu watumiaji wao kutumia huduma hii bila ya ada yeyote ile mwanzoni mwaka huu Soma hapa: Whatsapp bure sasa hakutakuwa na malipo. Mtandao huu unamilikiwa na wamiliki wa Facebook na unaongoza katika orodha ya mitandao ya kutumiana meseji kwa kuwa na watumiaji wengi zaidi.
No Comment! Be the first one.