Jana nilitembelea maonyesho ya Saba Saba, hasa hasa nilienda maeneo yanayodili ya teknolojia, ila kabla ya kufika huku nilipitia banda la BRELA, ambao ni wasajiri na watoaji leseni za biashara Tanzania. Habari njema ni kuwa www.teknokona.com sasa itakuwa chini ya Teknokona Solutions, huko mbele tunategemea kuwa na shughuli nyingine hii ni pamoja na kutoa huduma za ‘Social Media Management and Training’, hii huduma ya kuendesha akaunti za mitandao ya kijamii kwa niaba ya makampuni, watu mashuhuri n.k.
Airtel |
Nje ya hapo nilitembelea mabanda mbalimbali kama ya makampuni ya huduma za simu, kama Zantel na Airtel. Wale wanaotaka kununua simu ya Samsung Galaxy Pocket Edition basi inapatikana katika banda la Airtel kwa bei pungufu chini ya 199,000/= inayotangazwa kwingine kote.
Samsung |
Zantel |
Pia nilivutiwa na hili suala la kuweka mfumo wa kutumia gesi asilia katika magari, kwa habari alizotupa mhusika ni kwamba kwa sasa inaweza mgharimu mteja kati ya milioni 1 hadi 2 kutokana na mahitaji yako, ila kwenye bajeti ya serikali iliyopitishwa sasa vipuri vinavyotumika vimepunguziwa/ondolewa kodi hivyo wanategemea bei itapungua zaidi. Ghari lako likishafungwa mfumo huu utakuwa na uwezo wa kubadilisha na kuchagua kati ya kutumia mafuta au gesi hiyo mara moja kupitia kifaa kinachoweka pembeni tu ya usukani. Mambo ya Teknolojia hayo!!! Na kumbuka ingawa bei ya gesi kwa kilo ni ndogo zaidi kulinganisha bei ya lita moja ya mafuta, pia kilo moja hiyo ya gesi itaweza kwenda umbali mrefu zaidi kulinganisha na lita moja ya mafuta katika gari husika.
Gari Linalotumia Gesi na Mafuta |
Pia nilipita banda la TRA, kwa hapa kwa ufupi ni kwamba wale wakwepaji kodi wakae chonjo kwani TRA wanazidi kuja na vifaa vya kufanya zoezi hili liwe raisi zaidi kwa wateja wake.
Banda la Kampuni ya Pergamon Watoaji Vifaa vya Kodi za Mapato. |
Sehemu nyingine nilipopenda nilichojifunza leo ni upande wa Jeshi la Polisi, ukitoa hili la kuwa na tovuti yao itoayo habari mbalimbali zihusiyo masuala ya ulinzi na usalama pia wanatambua umuhimu wa sekta hii ya mtandao wa intaneti kwa kuwa na kitengo maalumu kinachoshughulikia makosa/wizi hufanywao kupitia intaneti (Cyber Crimes).
No Comment! Be the first one.