Kampuni ya OraSure ya nchini Marekani imepewa ruhusu kuingiza bidhaa yake ya kwanza sokoni itakayowawezesha wateja wake kujipima Ukimwi mahali popote watakapo.
Kupata ruhusu hiyo kutoka serikali ya Marekani kunaonekana ndio mwanzo mzuri wa bidhaa hiyo kupata ruhusu kwenye mataifa mengine duniani kote.
Watu wataweza kwenda maduka ya madawa na vifaa vingine vya tiba kununua kifaa hicho na kuweza kujipima mwenyewe na uhakika wa kupata majibu yako mwenyewe au na mtu utakaye ndani ya dakika 20 hadi 40. Kifaa hicho kinachoitwa OralQuick kitakuwa na kakifaa (a tester) kitakachotakiwa kugusishwa kwenye fizi au sehemu za kuta za shavu ndani ya kinywa.
Baada ya hapo utakiunganisha kwa kifaa kingine chenye mchanganyiko maalumu nao utakupa majibu yako ndani ya muda mchache (ndani ya dakika 20 hadi 40).
Je Kinapima Ukimwi Kwenye Mate?
Hapana, katika eneo la mdomo inasemekana kisayansi ndio sehemu yenye uwezekano mdogo kabisa wa kuwa na vidudu vya kusababisha Ukimwi. Hivyo kifaa hichi kinapima uwepo wa kinga flani za mwili ambazo mwili huwa huzitoa utakuwa unashambuliwa na vijidudu (H.I.V) vinavyosababisha ukimwi. Mtu akiambukizwa vijidudu vinavyosababisha ukimwi (H.I.V) mwili huwa unatengeneza na kuziachia kingamwili maalumu zinazopigana dhidi ya vijidudu hivyo.
Je Wewe Utanunua Kifaa hichi kikija?
Wanaharakati wa masuala ya Ukimwi wamegawanyika katika suala hili, wakati wengine wanasema hii itawafanya watu wengi zaidi wajue afya zao, wengine wanasema hii inaweza sababisha wengi kujiua kama majibu yatakuwa sio mazuri.
(Agosti, 2014 -KWA SASA ORAL QUICK ZINAPATIKANA DUNIANI KOTE)
No Comment! Be the first one.