Juzo tarehe 4, Tanzania kupitia Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia pamoja na Bwana David Sawe, Mtendaji Mkuu wa IBM Tanzania Ltd walisaini mkataba ushirikiano katika masuala mbalimbali yahusiyo teknolojia za kisasa kwa maendeleo ya Tanzania.
Chimbuko la makubaliano hayo Waziri alisema yalianza tangu mwaka 2007, kufuatia ziara ya kikazi ya Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wetu aliyoifanya nchini Marekani mwezi Septemba, 2007. Tangu hapo, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia ilichukua jukumu hilo la kuhakikisha makubaliano baina ya pande hizi mbili yanaanzishwa.
Maeneo hayo ni pamoja na:
Uanzishwaji wa kituo mahiri cha kumbukumbu za TEHAMA katika Chuo kikuu cha Dodoma,
Kuiwezesha Bandari ya Dar es Salaam kuweza kutoa huduma kwa ufanisi zaidi ili iwe kuwa
kiungo kikuu cha kutoa huduma za bandari kwa nchi jirani na Tanzania na kuwa chanzo
kikuu cha mapato ya Taifa,
kujenga na kuongeza uwezo wa kufanya tafiti mbalimbali katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela ya Arusha, kufanikisha majukumu ya
mtandao wa elimu na utafiti nchini, na kujenga kituo cha Teknolojia ya mtandao wa
TEHAMA (Cyber Park) na tafiti za elimu na serikali mtandao.
Hotuba ya iliyotolewa na Waziri husika inaweza patikana hapa!!!
No Comment! Be the first one.