Kampuni ya Samsung ya nchini Korea yaipiku Nokia katika kuwa muuzaji namba moja wa simu duniani. Nokia waliipiku Motorola mwaka 1998 kushika namba nafasi hiyo na sasa takribani miaka 14 baadae nao wamepokonya nafasi hiyo ya ‘market leader’ na kampuni ya Samsung.
Samsung imekuwa namba moja katika idadi ya simu ilizotengeneza na kuingiza sokoni, kwa kipindi cha miezi mitatu ya mwaka huu Nokia wameingiza idadi ya simu takribani milioni 82.7, Samsung wamesukuma mzigo wa Milioni 93.5. Ni ukweli tunaouona madukani na hata mitaani utumiaji wa simu za Samsung umekuwa unakua sana.
Je vipi kuhusu ‘Smartphones’? Smartphones ni aina ya simu zenye uwezo mkubwa kuzidi simu za kawaida zilizo na kazi chache, kama meseji, picha,video na ata matandao, lakini hivi vyote vinakuwa vya kawaida sana. Smartphones ni simu zenye uwezo mkubwa sana na zinaweza kutumika kwa kazi nyingi zaidi, mfano wa ‘Smartphones’ ni pamoja na simu za Blackberry, IPhone na pamoja na jamii za Samsung, HTC na Motorola.
Katika soko la Smartphones pia inasemekana Samsung wameipiku kampuni ya Apple, watengenezaji wa IPhone. Kutokana na watafiti wa Strategy Analytics ni Samsung ndo wanaongoza katika soko la ‘Smartphones’ kwa sasa, IPhone walisukuma mzigo wa milioni 35.1 wakati wakorea (Samsung) wanakuwa namba moja kwa kusukuma simu millioni 44.5.
Ushindi wa Samsung katika Smartphones umesaidiwa zaidi na simu zake za Galaxy, kwa sasa kampuni iliyokuwa inaongoza ya Nokia inashika namba 3 katika makundi yote mawili niliyoyazungumzia. Je wewe unaonaje katika hili? Natumia simu ya Blackberry lakini kwa kweli namezea mate simu za Galaxy kila napoziona hahahahahaha!!!!!!!! Nadhani Samsung inastahili, imeweka juhudi nyingi sana na sasa zinazaa matunda!!! Je ndo mwisho wa Nokia kuwa kiongozi? Tutaangalia mambo yatakuwaje miezi mitatu baadae!
Simu za Galaxy |
No Comment! Be the first one.