fbpx

OnePlus, simu, Uchambuzi

OnePlus yazindua Nord N10 5G na Nord N100! #Simu

oneplus-yazindua-nord-n10-5g-na-nord-n100-simu

Sambaza

Kampuni ya utengenezaji wa simu janja ya OnePlus wameweza  kuzindua simu janja mbili za bei ya kati, Kampuni hiyo imezindua simu janja toleo la Nord N10 5G na Nord N100.

Uwanja wa mahitaji ya watu kumiliki simu umezidi kuwa mpana zaidi kila kukicha na kufanya soko la simu janja kuongezeka maradufu zaidi kulinganisha na miaka ya nyuma.

Makampuni mengi makubwa yanayohusika na utengenezaji wa simu janja za bei ya juu  (flagship) yamekua yakiendelea kuzalisha simu za bei ya kati (midrange) ili kuteka soko zaidi.

Kwa wale wapenzi na wafuatiliaji wa simu janja kutoka kampuni ya OnePlus bila shaka hii ni moja ya habari nzuri kutoka OnePlus ambapo itawawezesha watu wenye kipato cha kawaida ama kati kuweza kumiliki simu hii janja na ya kisasa zaidi kutoka OnePlus.

INAYOHUSIANA  Mauzo ya simu janja za Huawei yaporomoka kwa 40% kutoka Mei kwenda Juni
OnePlus yazindua Nord N10 5G na Nord N100
OnePlus yazindua Nord N10 5G na Nord N100

Simu zote mbili zinaendeshwa mfumo wa uendeshaji wa Android 10 ilio na app ya muonekano wao spesheli unaotambulika kama Oxygen OS toleo la 10.5.             Muonekano wa OnePlus Nord N10 5G

Sifa za OnePlus Nord N10 5G

 • Teknolojia ya 5G 
 • Kioo ukubwa wa inchi 6.49
 • Kiwango cha kuburudisha cha 90HZ.
 • Kioo cha Corning Gorilla 3
 • Prosesa ya Qualcomm SM6350 Snapdragon 690
 • RAM ya 6GB
 • Uhifadhi wa ndani wa 128GB na uwepo wa kadi ya MicroSD.
 • Uwezo wa kutumia laini mbili
 • Mfumo endeshi wa Android 10, Oxygen OS 10.5. 
 • Ulinzi wa kidole (fingerprint)
 • Betri uwezo wa 4300mAh
 • Uwezo wa kuchaji kwa haraka 30W
 • Msaada wa kuchaji wa Warp Charge 30T. 
 • Kamera nne nyuma
     >64 MP, f/1.8, (wide)
     >8 MP, f/2.3, 119˚ (ultrawide)
     >5 MP, f/2.4, (depth)
     >2 MP, f/2.4, (macro)
 • Kamera ya mbele Megapixel 16
INAYOHUSIANA  Google Classroom yaboreshwa
                Muonekano wa OnePlus Nord N100

Sifa za OnePlus Nord N100

 • Teknolojia ya 4G
 • kioo ukubwa wa inchi 6.52
 • RAM ya 4GB
 • Prosesa ya Qualcomm SM4250 Snapdragon 420
 • Mfumo endeshi wa Android 10 Oxygen, OS 10.5
 • Uhifadhi wa ndani wa 64GB na uwepo wa kadi ya MicroSD.
 • Kamera tatu nyuma
   >13 MP, f/2.2, (wide)
   >2 MP, f/2.4, (macro)
   >2 MP, f/2.4, (depth)
 • Kamera ya mbele/selfi 8MP
 • Betri uwezo wa  5000mAh
 • Kuchaji haraka kwa 18W.
INAYOHUSIANA  Uhai wa tafiti za kisayansi nchini Uingereza

OnePlus Nord N10 5G itauzwa kwa takribani Tsh 987,000 hadi Tsh Milioni 1 (euro 360) na inakuja na rangi ya Midnight ice wakati Nord N100 itauzwa Tsh 550,000 hadi 570,000 (euro 200) na inakuja na rangi ya Midnight Frost. Kumbuka simu hizi zikipatikana nchini basi bei itapanda zaidi ya hii kwa sababu za kibiashara na kodi.

Chanzo: gadgets.com  gsmarena.com
Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Richard Kiwanga

Reply your comment

Your email address will not be published. Required fields are marked*