fbpx

Je, Umetumia DropBox?

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

DropBox ni njia nzuri ya kuweza kuwa na data zako kama mafaili ya ofisi, picha, video au muziki,  iwe ofisini, nyumbani, dukani au popote ulipo, muda wowote.
Mara nyingi katika ulimwengu wa sasa tunakuwa kwenye mishemishe na mara nyingi tunajikuta tumesahau kubeba vitu tunavyotakiwa kuwa navyo. Hii hali inatufanya tuwe na perfomance ndogo katika vitu muhimu na mara nyingi inatubidi tupoteze muda na pesa kufuata au kufuatilia vitu hivyo muhimu. DropBox inatuwezesha na inasaidia kupunguza aibu au adha hiyo.
DropBox inakurahisishia maisha. Kwa kutumia DropBox hautakuwa na ulazima wa kubeba laptop huku na kule, kwani ukiwa ume’install DropBox kwenye computer ya nyumbani, kazini na hata simu faili lolote utaloliweka utaweza kulipata sehemu zote hizi. DropBox itakuwa inali’copy kwenye account yako online na kulikopi tena kwa njia ya kulidownload kwenye folder lako la DropBox kwenye kifaa chako kingine.

Kiurahisi, DropBox inatumia mfumo wa cloud storage kukupa uwezo wa kuwa na data zako popote ulipo. Imerahisishwa zaidi kwa kukutumia faili la DropBox kwenye computer yako. Data zako zinawekwa katika account yako ya DropBox pale unaopo ‘dondosha’ data yako katika faili la DropBox. Hapo inapelekwa katika account yako ya DropBox iliyokuwa kwenye internet na kutumwa papo kwa hapo kwenye kila kifaa chako kinachotumia internet chenye huduma ya DropBox. Baada ya hapo unaweza kuangalia faili lako la excel, word au powerpoint na hata pdf au kuangalia movie au kusikiliza miziki yako kwa kudownload au kustream kwenye computer nyingine, tablet pc au simu yako. Kama ni document basi ukiifanyia mabadiliko ya aina yeyote itakuwa ikibadilishwa kwenye vifaa vyako vyote bila wewe kusumbuka.
DropBox inakupa nafasi zaidi ya kuweka vitu vyako na pia ‘back-up’ pale vifaa chako cha data kinapoharibika au kuibwa. Unapoanza na DropBox, unapewa 2GB za kuweka data zako inayoweza kufikia mpaka 18GB kwa kusaidia kuieneza DropBox kwa ndugu, jamaa na marafiki. Pia, unaweza kununua nafasi zaidi na huduma ya ‘DropBox for Teams.’ Kuna njia nyingine nyingi ambapo DropBox inaweza kurahisisha maisha yako. DropBox inakupa uwezo wa kumualika mwenzako kutumia faili unalokusdia katika akaunti yako huku mafaili mengine yakibaki ya kwako tu kuona na kutumia. Kwa kutumia huduma hii, wewe na ndugu, rafiki au mfanyakazi mwenzako mnaweza ku’share’ data na kuweza kufanya kazi pamoja.

DropBox kwenye wavuti

Ingawa uwezo wa huduma ya DropBox katika nchi yetu bado una changamoto, hasa kwa wale wenye intaneti yenye spidi ndogo, huduma hii bado ina uwezo wa kurahisisha mambo yako kwa data zenye kuchukua nafasi ndogo kama mafaili muhimu ya ofisi, katika usomi na maisha ya kawaida kama listi ya vitu vya kununua na kufanya.
Kama huduma nyingi zinazotumia mfumo wa intaneti, suala la msingi la kuangalia na DropBox ni usalama. DropBox ilipata matatizo mengi ya kiusalama mwanzoni ilpokuwa ikianza kukua na kujulikana na tangu kipindi hicho kampuni zinayoimiliki na kuifadhili DropBox zimepitia hatua nyingi kuhakikisha kuhakiki usalama wa huduma hiyo kufikia kiwango cha usalama unaotumiwa na benki katika kulinda data zako.
Kiufupi, DropBox ni njia rahisi na salama ya kuongeza perfomance katika ulimwengu wa sasa unaoonesha mwitiko mkubwa wa kurahisisha maisha kwa kutumia computer, smartphones na tablets na mfumo wa ulimwengu wa intaneti.  Unaweza sasa kujiunga na DropBox kwenye www.dropbox.com kwenye kifaa chako kinachotumia intaneti na kufaidi huduma hii.

DropBox kwenye simu yako.
Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  TCRA na sakata la kuonyesha chaneli za ndani
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

1 Comment

  1. Pingback: Dropbox wadukuliwa; Mamilioni ya akaunti hatarini - TeknoKona

Leave A Reply