fbpx
Anga, Drones, Tanzania, Teknolojia

Matumizi ya simu janja pamoja na ‘Drones’ katika kupambana na Malaria

matumizi-ya-simu-janja-pamoja-na-drones-katika-kupambana-na-malaria
Sambaza

Drones ambazo zinaenda sambamba na utumiaji wa simu janja katika ufanisi wa kile ambacho ilitengenezwa kufanya hivyo na Tanzania ni nchi mojawapo ambayo imeona ‘Drones’ zinaweza kuwana matumizi tofauti yale yaliyozoeleka.

Nchini Tnzania drones zinatumika katika kusaidia ulinzi wa hifadhi za wanyama pori ambao wamekuwa wakiwindwa na majangiri na kusababisha idadi ya wanyama hao ambao wengine hawapatikani nchi nyingine yoyote kupungua kwa kasi ya ajabu.

Drone ni ndege ambayo haiendeshwi na rubani isipokuwa inaendeshwa na kifaa maalum ya kuongozea (remote control) huku ndege hiyo isiyokuwa na rubani ikiwa imeunganishwa moja kwa moja na simu janja ambayo inatumika kama kioo kwa anayeiongoza ndege hiyo.

Mchango wa drones na simu janja katika kudhibiti ugonjwa wa malaria.

 Tanzania pamoja na Chuo Kikuu cha Aberystwyth kilichopo nchini Wales kupitia programu maalum ya kuondokana na malaria Tanzania Zanzibar imeamua kutumia ndrogoe zisizo na rubani (drones) katika kupambana na malaria ambayo ina uwezo wa kuzunguka na kumwaga dawa eneo kubwa ndani ya muda mfupi.

Drone aina ya Phantom 3 ina uwezo wa kuzunguka  eneo lote mathalani shamba kubwa la mpunga ndani ya dakika 20 tu . Hii inaonyesha kuwa matumizi ya ndege za namna hiyo zinaweza kufanikisha kumwaga dawa katika mazalia ya mbu wa malaria kwa haraka zaidi tofauti na kama wangetumika rasilimali watu kufanya kazi hiyo.

Ndege isiyo na rubani aina ya Phantom 3 yenye uwezo wa kuchua picha/video za kiwango cha 4K. Bei yake ni kuanzia $775|Tsh. 1,743,750.

Kuna mipango ya kutanua wigo wa programu ya kudhibiti ugonjwa wa malaria kwa kutumia drones ambapo itajumusha matumizi ya simu janja ambazo zitarekodi na kuweza kujua maeneo ambayo ni yana mazalia mengi ya mbu wanaoeneza malaria kisha kutoa taarifa kwa wahusika.

Drone Phantom 3 inaweza kutumika katika maeneo mengine (Tanzania bara) ila hofu ni kwamba drone ya Phantom 3 inaweza kuleta mkanganyiko na drones nyingine ambazo zinatumika kwenye masuala ya ulinzi kwenye mbuga za wanyama, uelewa kwa wakazi wa wanachi katika eneo husika kuepuka kuharibiwa.

Chanzo: Engadget

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Uzuri na ubaya wa 'selfie stick'.. ????????
2 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

2 Comments

  1. Drone ya kubebea mzigo wa zaidi ya kilo 200 yaundwa - TeknoKona Teknolojia Tanzania
    January 16, 2018 at 6:47 pm

    […] kuna sekta ambayo makampuni mbalimbali wanaiendeleza na kuzidi kukua kwa kasi huwezi kuacha kuongelea ndege zisizokuwa na rubani kwa matumizi yake kushamiri nchi nyingi duniani na kuwa kitega uchumi/chanzo cha mapato kwa […]

  2. Matumizi ya Drone kwa ajili ya kuokoa maisha - TeknoKona Teknolojia Tanzania
    January 19, 2018 at 4:01 pm

    […] zisizokuwa na rubani au maarufu kama “Drone” zimekuwa zikitumiwa kwa njia tofauti tofauti katika kufanikisha/kurahisisha jambo fulani na kuokoa muda kama njia nyingine ingetumika […]