Kwa watumiaji wote wa kawaida wa Windows XP muda wa kuanza kujifunza kuzoea Windows Vista na Windows 7 umewadia kwani Microsoft wametangaza kuanzia tarehe mwezi wa Nne mwaka 2014 ndo utakuwa mwisho wa ‘updates’ za aina zote kwa Windows XP.
Kwa maana nyingine ‘hackers’ na wadudu kama ‘virus’ na ‘trojans’ wapya kuanzia hapo watakuwa na uwezo mkubwa wa kuharibu ‘system’ ya Windows XP kwani Microsoft watakuwa wameachana na habari za msaada wa aina yeyote kama ‘security updates’ na zingenezo.
Windows XP iliingizwa sokoni mwaka 2001 na kampuni ya Microsoft ilishaacha kutoa copy mpya sokoni za Windows XP mwaka 2008 hii yote ili kutoa msukumo kwa watu kuhamia Windows Vista iliyokuwa imetolewa mwishoni wa mwaka 2006. Kwa miaka mingi Windows XP imekuwa inamiliki asilimia kubwa zaidi ya ‘operating system’ inayotumika kwenye komputa nyingi zaidi duniani. Mwaka 2009 zaidi ya asilimia 60 ya komputa zote duniani zilikuwa zinatumia Windows XP, baada ya umaharufu zaidi wa Windows 7 inasemekana kwa mara ya kwanza Windows XP imeshuka hadi nafasi ya pili mwishoni wa mwaka jana, kwa sasa Windows 7 ndo inatumika zaidi.
Lakini katika mashirika mbalimbali ya kibiashara na viwanda ni Windows XP bado inashikilia nafasi ya juu zaidi kwa zaidi ya asilimia 75 ya kumputa katika shughuli hizi zinatumia Windows XP.
Je wewe bado unatumia Windows XP? Unapendelea toleo gani la Windows na kwa nini? Tuambie kwa nini bado unaitumia au kwa nini umeihama…
No Comment! Be the first one.